Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) katika Ofisi za Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini
Dar es Salaam leo.
Mkuu wa Wilaya
ya Ubungo, Mhe. Kisare Makori akimkaribisha Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais- Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) kuzungumza katika kikao kazi na viongozi na watumishi wa
umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam wakati wa
ziara ya kikazi katika Manispaa hiyo leo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo (hawapo pichani) alipofanya ziara ya kikazi
katika Manispaa hiyo ili kupokea maoni, ushauri na kusikiliza kero za
watumishi wa umma leo Jijini Dar es Salaam.
Katibu wa
Chama cha TALGWU, Bw. Ibrahim Zambi akiwasilisha hoja mbalimbali
zinazowahusu watumishi wa umma wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi
ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah
J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya
watumishi wa umma wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo wakimsikiliza
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na
watumishi hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Askari
Msaidizi wa Manispaa ya Ubungo, Bw. Germini Massawe akiwasilisha
malalamiko kuhusu kada yake wakati wa ziara ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi wa umma wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Msaidizi-Idara ya Sera, Ofisi ya Rais-Utumishi, Bi. Loyce Lugoye
akifafanua jambo kuhusiana na masuala ya kiutumishi wakati wa kikao kazi
cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) na watumishi wa Halmashauri
ya Manispaa ya Ubungo kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waajiri nchini wametakiwa
kuzingatia mgawanyo sahihi wa Rasilimaliwatu katika Utumishi wa Umma ili
kuwa na utendaji bora na wenye matokeo katika utumishi wa umma.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Kairuki amesema mwajiri
anapoomba kibali cha kuajiri watumishi ni vema akazingatia mahitaji
kulingana na majukumu yaliyopo ili kuondoa ziada ya watumishi wa umma
wasio na kazi kuendana na fani walizosomea kwa lengo la kuwa na utendaji
mzuri.
“Ni vizuri sana wakati tunaomba
vibali vya kuajiri watumishi wa umma tukazingatia mgawanyo sahihi wa
rasilimaliwatu katika maeneo yetu kulingana na majukumu ya watumishi
tunaowahitaji badala ya kuomba watumishi wengi ambao wanasababisha kuwa
na ziada ambayo haitumika ipasavyo” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri Kairuki amesema katika
vibali 10,184 vilivyotolewa hivi karibuni na Ofisi ya Rais – Menejimenti
ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa,
Sekretarieti za Mikoa, Wakala za Serikali, pamoja na Taasisi na
Mashirika ya Umma ili kujaza nafasi zilizoachwa na watumishi wa umma
waliobainika kughushi vyeti vya elimu, Halmashauri ya Manisapaa ya
Ubungo imetengewa jumla ya nafasi 140.
Aidha, ameongeza kuwa,
Halmashauri hiyo imetengewa jumla ya nafasi za ajira mpya 397 kwa mwaka
wa fedha 2017/2018 hivyo zitendewe haki kwa kuhakikisha watumishi
watakaoajiriwa wanafanya kazi kwa mujibu wa mpango uliopo.
Mhe. Kairuki yuko katika ziara ya
kikazi katika mkoa wa Dar es salaama kwa lengo la kukutana na watumishi
wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto zinazowakabili
katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na kuleta
mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini ili kufikia malengo
yaliyopangwa na Serikali.
No comments:
Post a Comment