Monday, 10 July 2017

Upinzani Zimbabwe wamtaka Mugabe ajiuzulu


Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao
Vyama vya upinzani nchini Zimbabwe vimerejelea wito wao wa kutaka Rais Robert Mugabe mwenye umri wa miaka 93 ajiuzulu, na kumlaumu kwa kuiongoza nchi kutoka hospitalini kufuatia madai kuwa alisafiri kuenda Singapore kwa matibabu.
Gazeti la kibinfasi la News Zimbabwe lilimnukuu Obart Gutu, msemaji wa chama kikuu cha upinzani cha MDC akisema.
"yeye bado si kijana mdogo, njia hii anajiadhibu sio nzuri kwa afya yake ya kimwili na kiakili.
Mugabe ni lazima aondoke na aiache Zimbabwe kusonga mbele chini ya uongozi mpya."
Karauone Chihwayi, msemaji wa upande uliojitoa MDC naye alitoa matamshi kama hayo.
"Nchi hii imekwama leo hii kwa sababu rais wa Zanu anaongoza akiwa kitanda cha hospitali."

Chama cha Zanu-PF kimemteua bwana Mugabe kuwania urais mwaka ujao licha ya kuonekana kutokuwa na afya nzuri na amekuwa madarakani tangu mwaka 1980.

No comments:

Post a Comment