Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil
Mwambi akiwa na Mbunge wa Masasi Rashid Chuwachuwa (Kushoto) na Diwani
wa Kata ya Ndanda Costancia Bernad, wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa wakati alipo simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani
kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya
siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nanganga, wakati alipo simama,
akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya
kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amkabidhi Mbunge wa Jimbo la Ndanda Cecil Mwambi mipira, wakati alipo
simama katika kijiji cha Nanganga, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri
Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi wa kijiji cha Nanganga
wakimsikiliza Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipo simama katika
kijiji hicho, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani
Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Wananchi wa kijiji cha Mtama
wakishangilia Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, wakati alipo simama kuweka
jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo, akiwa njiani
kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya
siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akiteta jambo na Mbunge wa jimbo la Mtama,Nape Mnauye alipo
simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo,
akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya
kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Mtama, wakati alipo
simama kuweka jiwe la msingi katika kituo cha Polisi kijijini hapo,
akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya
kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akisalimiana na Mkurugenzi wa Shirika la Nyumba (NHC),wakati
alipofungua Zahanati katika kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea
Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
(katikati) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama Nape Mnauye Julai 13, 2017.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akikata utepe wakati alipofungua Zahanati katika kijiji cha
Mnolela, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa
ziara ya kikazi ya siku nne (kutoka kushoto) ni Mbunge wa Jimbo la Mtama
Nape Mnauye, Diwani Kata ya Mnolela Omar Liveta, Mkurugenzi wa Shirika
la Nyumba (NHC) kutoka kulia ni Meneja NHC Lindi Gibson Mwaigomole,
Meneja NHC Mtwara Nehemia Msigwa, Mkuu wa Mkoa Lindi Godrey Zambi Julai
13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akikagua wakati kifaa katika Zahanati ya Mnolela, baada ya
kuifungua, akiwa njiani kuelekea Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi
kwa ziara ya kikazi ya siku nne Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya
Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa,akizungumza na wananchi wa Mnolela mara baada ya kuifungua
Zahanati hiyo iliyopo katika Kijiji cha Mnolela, akiwa njiani kuelekea
Lindi, Waziri Mkuu yupo Mkoani Lindi kwa ziara ya kikazi ya siku nne
Julai 13, 2017. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
WaziriMkuu Kassim Majaliwa
ameupongeza uongozi wa Shirika la Nyumba (NHC) kwa kukamilisha ujenzi wa
zahanati ya kijiji cha Mnolela mkoani Lindi kwa muda mfupi.
Amesema ujenzi wa zahanati hiyo
ya kisasa mwezi Machi, 2017 na sasa tayari kimekamilika, jambo ambalo
litarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa eneo hilo na
wa jirani.
Waziri Mkuu alitoa pongezi hizo
jana jioni (Alhamisi, Julai 13, 2017) alipozungumza na wananchi wa
kijiji cha Mnolela baada ya kuzindua zahanati hiyo iliyosimamiwa na NHC.
Alisema ujenzi wa zahanati hiyo
ni muendelezo wa mkakati wa Serikali ya awamu ya tano wa kuboresha
huduma za afya kwa kusogeza huduma karibu kwa wananchi wake.
“Rais wetu Dkt. John Magufuli
amedhamiria kuwaondolea wananchi changamoto za mbalimbali zikiwemo za
huduma za afya, hivyo tuendelee kumuunga mkono.”
Kwa upande wake Mkurugenzi wa
NHC, Bw. Nehemia Mchechu alisema mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo
ulisimamiwa na NHC na umegharimu sh. milioni 65.5.
“Shilingi milioni 15 zilitolewa
na Rais. Dkt. Magufuli, sh. milioni 10 zilitolewa na Mheshimiwa Mbunge
wa jimbo la Mtama, Nape Nnauye, NHC ilitoa sh. milioni 10 na kiasi
kilichosalia ni mchango wa halmashauri.”
Awali Mbunge wa jimbo la Mtama,
Mheshimiwa Nape alimshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa mchango mkubwa
alioutoa katika mradi wa ujenzi wa zahanati hiyo.
Mheshimiwa Nape alisema zahanati
hiyo ni mkombozi kwa wakati wa kijiji cha Mnolela na wananchi wengine
wanaoishi kwenye maeneo yaliyo jirani na kijiji hicho.
No comments:
Post a Comment