Monday, 17 July 2017

Uchumi wa China wakua

Uchumi wa China ulikua kwa asilimia 6.9 kati ya mwezi Aprili na Juni kwa mujibu wa takwimu rasmi ambayo ni asillimia ya ju kuliko ilivyotarajiwa.
Ukuaji huo ambao ni mkubwa ukilinganishwa na miezi mitatu iliyopita ulikuwa sawa na robo ya kwanza ya mwaka 2017.
Wachanganuzi wengi walitarajia uchumi wa china kupunguza mwendo wa ukuaji wake.
Lakini takwimu za hivi punde ziko juu kuliko matarajio ya ukuaji wa asilimia 6.5.
Licha ya jitihada za kupunguza uwekezaji katika nyumba, uwekeza katika sekta za ujenzi ulikua kwa asilimia 8.5 katika robo ya kwanza ya mwaka, ambayo ni juu kutoka kipindi kama hicho mwaka 2016.

Wadadisi wanatabiri kuwa sheria ngumu za ukopeshaji haziwezi kuathiri uwekezaji kama wengi walivyotarajia.

No comments:

Post a Comment