Tomothy
Weah amefuata nyayo za babake ambaye ni mshindi wa taji la Ballon d’Or
George Weah baada ya kutia saini kandarasi na klabu ya Paris St-
Germain.
Mshambuliaji huyo wa miaka 17
ametia saini mkataba wa miaka 3 na PSG klabu ambayo George Weah
aliiwakilisha kutoka mwaka 1992 hadi 1995.
Tayari kumekuwa na uvumi kwamba mwana anafuata nyayo za babake.
Mnamo mwezi Septemba 2016, kinda
Weah alifunga hat-trick katika ushindi wa 8-1 dhidi ya klabu ya
Ludogorets katika mechi yake ya kwanza ya Uefa.
”Ni fahari kubwa kuendeleza pale
baba alipowachia” , alisema Weah ambaye alizaliwa mjini New York na
kujiunga na New York Red Bulls kabla ya kujiunga na chuo cha mafunzo ya
soka cha PSG mnamo mwezi Julai 2014.
”Niko katika klabu kubwa na natumai nitaendelea kuimarika ili niweze kuichezea timu kubwa”.
Babake mwenye umri wa miaka 50
kutoka Liberia aliwahi kushinda mara tatu taji la mwanasoka bora wa
Afrika na mchezaji wa pekee wa Afrika kuwahi kushinda taji la Ballon
d’Or mwaka 1995.
Alijipatia umaarufu katika klabu ya Monaco 1988 na kufanikiwa kuzichezea PSG na AC Milan muongo uliofuata.
Pia aliichezea Chelsea na Manchester City katika ligi ya Uingereza katika miaka ya mwisho ya soka yake.
No comments:
Post a Comment