Hatua hiyo imetokana na serikali ya nchi hiyo kuingilia masuala ya soka hivi karibuni ambapo ni kinyume na sheria za Shirikisho hilo.
Kwa mujibu wa ratiba iliyotolewa na CAF, timu ya El Merreikh na Al Hilal Omdurman zilizokuwa Kundi A zimewekwa kando huku michuano ya robo fainali inatarajiwa kukuwakutanisha Al Ahli Tripoli dhidi ya Esperance, Ferroviario da Beira imepangwa na USM Alger, Al Ahly itakutana na Etoile du Sahel wakati mabingwa watetezi Mamelodi Sundowns FC wakipangwa kuanzia nyumbani dhidi ya Wydad Casablanca kutokana na droo iliyochezeshwa na CAF.
Ratiba ya michuano ya ligi ya mabingwa Afrika iliyotolewa na CAF kupitia ukurasa wake wa twitter.
Kwa mujibu wa ratiba hiyo, mechi za robo fainali zitapigwa mwezi
Septemba, nusu fainali itakuwa Oktoba na fainali itapigwa mwezi Novemba
mwaka huu.
No comments:
Post a Comment