Tuesday, 18 July 2017

Sudan Kusini yatangaza hali ya hatari


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza hali ya hatari kaskazini magharibi mwa nchi.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir ametangaza hali ya hatari kaskazini magharibi mwa nchi.
Taarifa iliyotangazwa na televisheni ya taifa haikutoa sababu ya kutangzwa kwa tahadhari hiyo.
Tahadhari hiyo inatarajiwa kusalia kwa kipindi cha miaka mitatu.
Mzozo wa Sudan Kusini umesababisha vifo vya maelfu ya watu na kuwalazimu wengine zaidi ya milioni mbili kuhama makwao tangu mwaka 2013.
Tahadhari ya kwanza ilitangazwa mwaka 2014 katika jimbo la Unity lililo kaskazini na lile la Jonglei lililo mashariki wakati waasi walipigana na vikosi vya serikali.
Msukosuko unashuhudiwa pande zote na mapigano yamesambaa hadi mashariki mwa nchi.
Umoja wa Matiafa unasema kuwa maelfu ya raia wamekimbia mji wa Pagak na maeneo yaliyo karibu, na kuvuka mpaka kuingia Ethiopia. Watoa misaada nao pia wamelazimika kuhama.

No comments:

Post a Comment