Wednesday, 19 July 2017

PSG yapania Kuvunja Rekodi kwenye Usajili wa Neymar


Katika kuonesha jeuri ya pesa matajiri wa kiarabu wanaoimiliki klabu ya PSG wamepiga hodi katika klabu ya Barcelona tayari kwa ajili ya kuvunja rekodi ya dunia kumtwaa mshambuliaji wa klabu hiyo Neymar.
Taarifa zinasema kiasi cha zaidi ya £200m ambayo ni mara mbili na zaidi ya pesa zilizotumika kumnunua Paul Pogba ambaye kwa sasa ndio anashikilia rekodi ya usajili ya dunia kwa sasa.
Ripoti zinasema klabu ya PSG inataka kutumia mwanya wa Neymar kukosa uhuru wa kucheza free mbele ya Messi hivyo wanataka kutuma ofa ya karibia £222m ambayo ni wazi itawashawishi Barcelona kumuuza.
Katika dili hiyo Neymar atakula £30m kila mwaka na uwepo wa Dani Alves katika kikosi cha PSG unaweza kuwa ushawishi mkubwa kwa Neymar na PSG wanaweza kumtumia mlinzi huyo kumshawishi Neymar.
Habari zinasema Neymar hana furaha na Barcelona kwani ni ngumu kuchukua tuzo ya Ballon D’Or ukicheza mbele ya Suarez na Messi ambapo washambuliaji hao wanaminya uhuru wa Neymar akiwa uwanjani.
Lakini klabu ya Barcelona yenyewe wamesema hawana mashaka hata kidogo kuhusu kuondoka kwa Neymar kwani suala hilo katika soko la usajili ni gumu kutokea na wao wanapuuza uvumi wote kuhusu Neymar.

Josep Vives msemaji wa klabu ya Barcelona amesema “hata hatuwazi kuhusu hilo kwani ni ngumu kutokea, ni mchezaji wetu muhimu sana na sidhani kama tunaweza kupokea ofa yoyote juu yake.”

No comments:

Post a Comment