NA CHRISTINA MWAGALA, OFISI YA MEYA WA JIJI
MSTAHIKI Meya wa
Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita ametoa mwezi mmoja kwa wafanyabiashara
wa vizimba vya standi ya mabasi Ubungo kulipa kodi na kusisitiza kuwa
iwapo watakaidi agizo hilo, ataagiza Polisi kuwaondoa kwa nguvu.
Mstahiki Meya Mwita
ametoa agizo hilo leo alipofanya ziara ya kushtukiza katika standi ya
mabasi ya Ubungo ikiwa ni baada ya kupokea taarifa kuwa kuna
wafanyabiashara hawataki kulipa kodi.
Katika ziara hiyo
Meya Mwita aliambatana na Kamati ya Fedha na uchumi ya jiji ambapo
kabla ya kutoa maamuzi hayo, a litoa nafasi kwa wafanyabiashara
kuzungumza kuwa ni kwanini hawataki kulipa kodi , na hivyo baada ya
kupokea maelezo hayo alifikia hatua ya kutoa maamuzi hayo.
Meya Mwita alisema
kuwa jambo la wafanyabiashara hao kugoma kulipa kodi ambazo wanapaswa
kulipa, ni kulikosesha jiji mapato ambayo yangeweza kutumia kwenye
shughuli za Maendeleo na kusisitiza kuwa wasitake kuingia kwenye mgogoro
na jiji.
” Ndugu zangu sasa
mmeanza kunipa wasiwasi mkubwa, lakini pia mnataka kunilazimisha nitumie
utaratibu wa kutangaza tenda zakuingia humu ndani kufanya biashara
zenu, jambo ambalo kwa silimia 100 najua hamtapata, na wote hapa
mnategemea kupata chochote hapa, sasa msitake nifike huko.
Hizi pesa ambazo
mnalipa hapa, ndio zinatumika kufanya usafi hapa, lakini pia pesa hizo
hazina kazi moja tu, sasa mkisema hamtaki kulipa mnataka hii stendi
hapa ijiendeshe vipi?, sasa naagiza hadi kufikia mwishoni mwa mwezi wa
nane, muwe mmeshalipa kodi, vinginevyo polisi watawaondoa hapa.
Alisisitiza kuwa,
msije kushangaa, hapa Polisi wanawaondoa kwa nguvu, na polisi Ikifika
muda huo ambao nimeutoa halafu ikatokea pesa hazijalipwa, hawa watu hapa
nisiwaone”aliagiza Meya Mwita.
Hata hivyo katika
hatua nyingine aliwataka watumishi wa standi ya Ubungo kuwa na kauli
nzuri kwa wafanyabiashara sambamba na kuonyesha ushirikiano huku pia
akionya wafanyabaishara namkuwataka waonyeshe ushirikiano kwa watendaji
walipo kwenye standi hiyo.
No comments:
Post a Comment