Sehemu ya watumishi wa umma wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe wakimsikiliza Waziri
wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala
Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na watumishi
hao kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) akizungumza na viongozi na watumishi wa umma wa Halmashauri
ya Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe (hawapo pichani) leo alipofanya
ziara ya kikazi katika Kata hiyo ili kupokea maoni, ushauri na
kusikiliza kero za watumishi wa umma Jijini Dar es Salaam.
Mhudumu wa Afya kutoka Hospitali
ya Magomeni Bii. Rukia Mkapa akitoa malalamiko yake wakati wa ziara ya
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na
watumishi wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mwalimu Paschal Mugayana kutoka
shule ya Sekondari ya Njechele akitoa malalamiko yake wakati wa ziara
ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki (Mb) wakati wa kikao kazi na
watumishi wa umma wa Kata ya Kawe kilichofanyika leo Jijini Dar es
Salaam.
Ofisi ya Rais – Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora inaendelea kusanifu na kuboresha Mfumo
wa Taarifa za Kiutumishi na Mishahara (HCIMS) ili uweze kutumika kutoa
taarifa za msingi kwa watumishi wa umma wengi zaidi kwa lengo la kuleta
mabadiliko ya utendaji kazi katika sekta ya umma nchini.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J.
Kairuki (Mb) amesema hayo leo katika kikao kazi na Watumishi wa Umma wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni – Kata ya Kawe, jijini Dar es
Salaam.
Mhe. Kairuki amesema Mfumo wa
HCIMS awali ulikuwa unapatikana Ofisi ya Rais–Utumishi pekee, lakini
baadae ukakasimishwa kwa Maafisa Utumishi lakini sasa lengo ni kuwafikia
watumishi wa umma waweze kuona taarifa zao ili kupata taarifa sahihi na
za uhakika katika kanzidata. Amesema Tovuti ya Watumishi, Watumishi Portal, imeanzishwa maalum ili watumishi wa umma wajisajili kupitia tovuti ya Ofisi ya Rais-Utumishi yenye anuani www.utumishi.go.tz na kuona taarifa zao za msingi.
Waziri Kairuki, pamoja na hilo,
amesema mfumo wa HCIMS umegatuliwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa
hivi sasa ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kufanya maamuzi kwa
haraka zaidi.
“Kwa kuwa mahitaji ya watumishi
wa umma ni mengi hivyo tumeona ni vema tukakasimu Mfumo huu na kwa
watumishi wa umma katika kada nyingine ili kurahisisha utendaji kazi na
kuleta mabadiliko” Mhe. Kairuki amesema.
Waziri Kairuki ameongeza kuwa
tayari mafunzo kuhusu namna ya kutumia mfumo yalikwishatolewa kwa
Maafisa Elimu na Makatibu wa Afya wapatao 633.
“Tumeamua kuanza na sekta hizi
kwa sababu ni sekta zenye watumishi wa umma wengi zaidi ukilinganisha na
sekta nyingine lakini tutaendelea kugatua mfumo wa HCIMS ili ufike
katika sehemu nyingi zaidi za kutolea huduma (Service Delivery Points).” Mhe. Kairuki ameongeza.
Mhe, Kairuki yuko katika ziara ya
kikazi katika mkoa wa Dar es Salaam, ambapo leo ni siku yake ya tano
aliyoitumia kukutana na Watendaji na watumishi wa umma wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni-Kata ya Kawe.
Lengo la ziara ni kukutana na
watumishi wa umma na kusikiliza malalamiko, ushauri na changamoto
zinazowakabili katika maeneo yao ya kazi ili kuweza kuzifanyia kazi na
kuleta mabadiliko katika Utumishi wa Umma nchini.
No comments:
Post a Comment