Korea Kaskazini imerusha kombora jingine la masafa marefu kutoka jimbo
lake la magharibi kulingana na mamlaka ya Japan na Korea Kusini.
Kombora hilo lilirushwa kutoka Bangyon Kaskazini mwa mkoa wa Pyongan
kulingana na chombo cha habari cha Yonhap kikitaja duru za jeshi la
Korea kusini.
Tokyo imesema kuwa kombora hilo huenda lilianguka katika eneo la kiuchumi la bahari ya Japan.
Korea Kaskazini imeongeza viwango vya majaribio vya makombora yake
katika meizi ya hivi karibuni hatua inayoendelea kuzua wasiwasi.
Kombora hilo la siku ya Jumanne lilisafiri umbali wa kilomita 930 kwa dakika 40,kulingana na Korea Kusini na Japan.
Hili ni kombora la 11 lililogunduliwa mwaka huu lakini urefu wake
umeongezeka kulingana na mwandishi wa BBC mjini Seoul Stephens Evans.
Mara ya mwisho Korea Kaskazini ilifanyia majaribio kombora lake mnamo mwezi Mei.
Ilirusha makombora yake katika wakati tofauti, yote yakielekezwa bahari ya Japan.
No comments:
Post a Comment