Saturday, 15 July 2017

Habari Picha

PIX 1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimuangalia mhamiaji haramu katika dirisha dogo la chumba cha mahabusu, Kituo cha Polisi Pangani mkoani Tanga. Mhamiaji huyo kutoka nchini Somalia alikamatwa wilayani Pangani katika mwambao wa Bahari ya Hindi. Masauni akiwa mjini Tanga aliwaagiza Maafisa Uhamiaji na Polisi kuongeza kasi ya kutafuta mizizi ya wahamiaji haramu mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Kituo Polisi mjini Pangani, Christina Musyani. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani wakati alipokua anamfafanulia masuala ya ulinzi na usalama wilayani humo. Masauni alikikagua kituo hicho pamoja na nyumba za askari polisi ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kulia) akimsikiliza Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Wilaya ya Pangani, mkoani Tanga, Christina Musyani alipokuwa anamuonyesha moja ya nyumba ambazo zipo katika hali mbaya zaidi kutokana na kutofanyiwa matengenezo kwa muda mrefu. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akitoka kulikagua Gereza la Wilaya ya Pangani mkoani Tanga. Masauni pia alizungumza na mahabusu wa Gereza hilo kwa kusikiliza kero zao na kuzitolea maamuzi hapo hapo na baadhi kuahidi kuzifanyia kazi kwa haraka zaidi. Kwa nyuma ni Mkuu wa Gereza hilo, Elishinikizo Moshi. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akimsalimia Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu, wakati Naibu Waziri huyo alipowasili wilayani Muheza mkoani Tanga kwa ajili ya ziara yake ya kikazi. Katikati ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Mhandisi Mwanaasha Tumbo. Kulia ni Mkuu wa Gereza Muheza ambalo ujenzi wake unatarajiwa kujengwa hivi karibuni baada ya Masauni kuamuru ujenzi huo uanze  mara moja.  Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
PIX 6
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akimsikiliza Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhandisi Mwanaasha Tumbo alipokua anatoa taarifa yake ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo. Mara baada ya kusomewa taarifa hiyo na kuona kuna changamoto mbalimbali ikwemo ya kutokuwepo Gereza wilayani humo, Masauni aliamuru ujenzi wa Gereza hilo uanze mara moja ikiwa mahitaji yote ya nguvu kazi na mengineyo yapo. Wapili kulia ni Mbunge wa Jimbo la Muheza, Balozi Adadi Rajabu.  Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

No comments:

Post a Comment