KLABU ya Arsenal imekubaliana na Lyon kumsajili mshambulaji Mfaransa,
Alexandre Lacazette kwa dau ambalo linaweza kuwa la rekodi, Pauni
Milioni 44.
Dili hilo litavunja rekodi ya usajili wa Pauni Milioni 42.5 ambazo
Arsenal ilitumia kumsajili Mesut Ozil kutoka Real Madrid mwaka 2013 na
inatarajiwa kukamilisha uhamisho wake ndani ya saa 48 zijazo, baada ya
Lacazette kusafiri kwenda London kwa vipimo.
Arsenal ilijaribu bila mafanikio kutuma ofa ya Pauni Milioni 29
kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 mwaka mmoja uliopita na
sasa imepandisha dau hadi Pauni Milioni 39.5 ambazo awali zilikataliwa
kabla ya kufikia makubaliano na mmiliki wa Lyon, Jean-Michel Aulas.
Alexandre Lacazette (kulia) amekwenda London kufanya vipimo vya afya
tayari kukamilisha uhamisho wa dau la rekodi Arsenal, Pauni Milioni 44Lacazette amekuwa na Lyon tangu anaanza soka yake ya ushindani akiigungia mabao 129 katika mechi 275 timu hiyo ya nyumbani kwao. Msimu uliopita alifunga mabao 37 katika mechi 45.
No comments:
Post a Comment