Sunday, 2 July 2017

Al-Qaeda yawaonyesha mateka kwenye video Mali

 Kikundi cha mtandao wa al-Qaeda kinachoendesha shughuli zake nchini Mali, kimetoa kanda ya video cha mateka 6 wakati rais wa Ufaransa Emmanuel Macro akifanya ziara nchini humo.
Mateka hao ni pamoja na mfanyakazi mmoja wa shirika lisislo la serikali na dakari mmoja mzee raia wa Australia.
Hakuna mazungumzo rasmi ya kuachiliwa mateka hao yamefanyika.

Bwana Macro yuko nchini Mali kuzungumzia kuundwa kikosi cha kanda kitakacho pambana na wanamgambo.
Akiongea mjini Bamako Macro alisema kuwa Ufaransa na nchi tano za Sahel zikiwemo, Mali, Burkina Faso, Chad, Mauritania na Niger, zinatakiwa kufanya kazi pamoja kuwaangamiza magaidi.
Kati ya mateka walio onyeshwa kwenye kanda hiyo ni pamoja na Sophie Petronin, ambaye alitekwa nyara mwezi Desemba katika mji Gao, ambapo alikuwa akiongoza shirika lisilo la serikali lililokuwa likiwasaidia watoto walio na utapiamlo.
Aliyezungumza kwenye video hiyo alisema kuwa Bi Petroni alikuwa na matumaini kuwa bwana Macro atasaidia kurejea kwa familia yake.,


No comments:

Post a Comment