Kutokana na uchovu wa kutafuta maji, wanawake mkoani Mara hushindwa kuwapa unyumba waume zao.
Hayo yamesemwa leo Jumatatu na Mbunge wa Viti Maalum mkoani humo, Agnes Marwa alipokuwa akichangia bajeti ya Serikali bungeni.
"Ikifika jioni, wanawake mkoani Mara hushindwa kuwapa unyumba waume zao.
Naomba Serikali iangalie namna ya kumtua ndoo mwanamke," amesema Agnes.
Uhaba wa maji ni hoja iliyoibuliwa na wabunge wengi wanaoitaka Serikali
kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya miradi yake ili kumaliza kero
hiyo.
Serikali imeshauriwa kuimarisha mfuko wa maji vijijini kwa kutafuta vyanzo vya uhakika vya mapato ili kufanikisha hilo.
No comments:
Post a Comment