Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakijadili kwa umakini
na katibu mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Mpoki Ulisubisya wakati wakiongea na
waandishi wa habari(Hawapo kwenye picha) juu ya taarifa ya kuibiwa kwa
mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma katika hospitali ya Temeke jijini Dar Es
salaam.
Mganga Mkuu wa Serikali Prof.
BaKari Kambi akitoa ufafanuzi mbele ya waandishi wa habari (Hawapo
kwenye picha) wakatati wa uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za kuibiwa
kwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliofanyika mapema leo katika Ofisi
ndogo za Wizara jijini Dar Es Salaam.
Waandishi wa habari wa vituo
tofauti wakifuatilia kwa umakini uwasilishwaji wa taarifa ya tuhuma za
kuibiwa mtoto mmoja wa Bi Hasma Juma uliowasilishwa leo na mwenyekiti wa
kamati Dkt. Charles Majige ambae pia ni Daktari bingwa wa Magonjwa
yakina mama , uliofanyika leo mapema katika ofisi ndogo za Wizara jijini
Dar Es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Mpoki Ulisubisya
akijibu maswali yaliyoulizwa na Waandishi wa Habari juu ya tuhuma za
kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi.Hasma Juma katika Hospitali ya Temeke
jijini Dar es salaam.
Mwakilishi wa familia ya Bi Hasma
Juma Jordan Jaddah akifuatilia kwa umakini Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Ummy Mwalimu wakati akisisitiza juu
ya taarifa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa kamati ya Uchunguzi Dkt.
Charles Majige juu ya kuibiwa kwa mtoto mmoja wa Bi. Hasma Juma.
NA WAMJW DAR ES SALAAM
WAZIRI wa Afya, Maendeleo ya
Jamii,Jinsia Wazee na Watoto Ummy Mwalimu amepokea taarifa kutoka kwa
tume huru aliyoiunda ili kuchunguza malalamiko ya Bi. Asma Juma kuhusu
kuibiwa mtoto mmoja kati ya mapacha wawili katika hospitali ya Rufaa ya
Temeke Dar es salaam.
Akipokea taarifa kutoka kwa
Mwenyekiti wa tume hiyo Daktari bingwa wa magonjwa ya kinamama Dkt.
Charles Majige Waziri Ummy amesema kuwa Bi. Asma Juma(29) hakuwa na
watoto mapacha kama ilivyodaiwa na mlalamikaji huyo kutokana na kipimo
cha Utra sound kukosea katika uchukuaji picha ya mtoto akiwa tumboni.
“Nimepokea taarifa kutoka kwa tume
huru niliyoiunda hivi karibuni na imethibitisha kuwa Bi. Asma Juma
hakuwa na watoto mapacha ila uchukuaji mbaya wa picha ya mtoto aliyekuwa
tumboni uliofanywa katika zahanati ya Huruma ukatoa matokeo hayo”
alisema Waziri Ummy.
Aidha Waziri Ummy amesema kuwa
wanafamilia ya Bi. Asma wanatakiwa kumfariji ndugu yao na sio
kumkumbushia jambo hili mara kwa mara kwani litamharibu kisaikolojia na
kushindwa kutekeleza wajiu wake kwa mtoto kama mama mzazi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
kamati hiyo Dkt. Charles Majige Amesema kuwa Bi. Asma aliamini hivyo kwa
sababu Hospitali ya temeke hawakumchukua vipimo vya picha bali
walitumia taarifa ya vipimo vya awali .
Aidha Dkt. Majige Amesema kuwa
tume hiyo imebaini kuwa Bi. Asma hakuibiwa mtoto na alikua hana mapacha
kwa sababu uzito wake ulikua sio wa kubeba watoto wawili na katika
chumba cha upasuaji kulikua na wataalamu 6 kutoka vitengo mbalimbali.
Kwa upande wake mwakilishi wa
Familia ya Bi. Asma Juma Jordan Jaddah amesema kuwa anaishukuru Serikali
kupitia Wizara ya Afya kufatilia jambo hilo kwa ukaribu na kupata
ukweli wa malalamiko yao na wameikubali taarifa hiyo .
“Tunaipongeza tume hiyo chini ya
Wizara ya Afya na tunashukuru kwa msaada wao mwanzo mpaka mwisho na
kutupatioa majibu ya kuridhisha nasi tutakuwa bega kwa bega katika
kumfariji ndugu yetu kwa jambo hili lilitokea” alisema Bw. Jaddah.
Mbali na hayo Waziri Ummy
amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli kwa maagizo ya kila mtoto wa kike atakaepata ujauzito shuleni
asirudi shuleni ila aendelee na masomo mengine ya ujuzi.
No comments:
Post a Comment