Afisa Utumishi Manispaa ya Ubungo Ndg Alute Joseph akitoa ufafanuzi wa kanuni za maadili ya Utendaji katika Utumishi wa Umma
Leo June 20, 2017 watumishi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo
wameanza kuadhimisha wiki ya Utumishi wa Umma kwa kufanya mkutano mkubwa
uliohudhuriwa na watumishi wote wa makao makuu katika ukumbi wa
Manispaa hiyo mkutano ambao umeongozwa na Afisa Utumishi Mkuu wa
Manispaa hiyo Ndg Ally Juma Ally kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya
Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo.
Akiongea katika kikao hicho mara baada ya kufungua kikao Afisa
Utumishi mkuu aliwajulisha kuanza rasmi kwa wiki ya utumishi na kutoa
utaratibu wa jinsi Halmashauri itakavyotimiza maadhimisho hayo ambapo
alisema kuwa kwa wiki hii ya maadhimisho muda wa kutoka kazini
utaongezeka kwa saa moja badala ya kutoka saa tisa na nusu mchana
itakuwa ni saa kumi na nusu, hali kadhalika alisisitiza mambo ya
kuzingatia katika wiki hii na hata baada ya maadhimisho no pamoja na
Kufanya kazi kwa kuzingatia sheria,kanuni taratibu na miongozo
mbalimbali ya utumishi wa umma, Kufanya kazi zetu kwa kuzingatia maadili
ya utumishi wa umma, na Kufanya kazi kwa uadilifu mkubwa bila ya
viashiria vya kupokea rushwa au hongo katika kutoa huduma katika ofisi
za serikali au umma.
Mengine ni Kuongeza Ari na kujituma katika kutekeleza majukumu
yetu, Kufanya kazi kwa maarifa na kuwasikiliza wanaanchi wanapofika
kupata huduma katika ofisi za umma/serikali na Kuweka vizuri kumbukumbu
za wananchi watakaohudumiwa kwa kipindi hiki ili kuzitolea taarifa
kwenye mamlaka husika.
Pia wamesisitizwa kutoa Huduma bora, Utii kwa serikali, Kuongeza
bidii ya kazi, Kutoa huduma bila upendeleo, Kufanya kazi kwa Uadilifu,
Uwajibikaji kwa Umma, Kuheshimu sheria na taratibu za kazi, na Matumizi
sahihi ya Taarifa.
IMETOLEWA NA:
KITENGO CHA HABARI NA UHUSIANO
HALMASHAURI YA MANISPAA YA UBUNGO
No comments:
Post a Comment