Na Octavian Kimario-WHUSM Dodoma.
Wazo la kuwarudisha nchini
Dinosaria halina tija kutokana na ugumu wa Kiteknolojia na gharama
ikilinganishwa na faida za kuchukua hatua hiyo.
Akijibu swali la Mbunge wa
Mchinga Mhe. Hamidu Hassan Bobali lililo uliza,Ni nini kauli ya mwisho
ya Serikali kuhusu faida ambayo wananchi wa Lindi na Tanzania kwa ujumla
wananufaika kutokana na mabaki hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii Mhe. Ramo Makani amesema Tanzania itaendelea kusisitiza kupata
manufaa kutokana na uwepo wa Dinosaria wake huko Berlin-Ujererumani.
“Kufuatia majadiliano ya kina
yaliyohusisha wataalamu wabobezi katika masuala ya Malikale kutoka pande
zote mbili imekubalika kuwa Serikali ya Ujerumani itaendesha shughuli
za utafiti zaidi huko Tendaguru na katika maeneo jirani ili kuwezesha
uchimbaji wa mabaki ya Dinosaria wengine yanayoaminika kuwepo katika
maeneo hayo pamoja na kuanzisha Kituo cha Makumbusho ili shughuli za
Utalii zifanyike katika eneo hilo na kuvutia watalii kutoka nchini na
nje ya nchi” alisisitiza Mhe. Makani.
Kuhusu Serikali kupunjwa mapato
yatokanayo na viingilio katika Makumbusho ya Elimu Viumbe ya
Berlin,Mhandisi Makani amesema jambo hilo halina ukweli wowote kwani ni
ngumu kufahamu ni kiasi gani hupatikana kama kiingilio kuwaona Mijusi
kutoka Tanzania kwakuwa Makumbusho hiyo ina kumbi nyingi zenye masalia
kutoka nchi mbali mbali za Afrika na gharama za kuendesha Makumbusho
hiyo hutolewa na Serikali ya Ujerumani.
Ameeleza kuwa Serikali ya
Ujerumani itafadhili zoezi la uimarishaji idara inayohusika na Malikale
katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kuwezesha upatikanaji wa
wataalamu wa kutosha wa fani husika ilikuendeleza Utalii wa Malikale
nchini.
Mijusi mikubwa (Dinosaria)
ilichimbwa katika Kilima cha Tendaguru,mkoani Lindi kati ya waka 1909 na
mwaka 1913 na kupelekwa katika makumbusho ya Elimu Viumbe ya Berlin
nchini Ujerumani.
No comments:
Post a Comment