Chile imetinga fainali ya Kombe la Mabara kwa ushindi wa mabao 3-0, yote kwa mikwaju ya penalti baada ya dakika 120 za 0-0.
Kipa Bravo ambaye pia anadakia Man City, ndiye ameibuka shujaa baada ya
kupangua penalti tatu huku Ronaldo akiwa anasubiri kupiga yake
"baadaye".
Mchezo ulikuwa mgumu sana kama ulivyotarajiwa kati ya mabingwa wa Ulaya
timu ya taifa ya Ureno dhidi ya Chile ambao ni mabingwa wa America.
Mchezo huo wa nusu fainali ya confedaration cup ulimalizika dakika 90
kukiwa hakuna timu iliyopata bao na hata zilipoongezwa 30 ili kumalizia
120 milango bado ilikuwa ni migumu.
Baada ya hapo muamuzi aliamuru kupigwe mikwaju ya penati ambapo ndio
Ureno waliondolewa baada ya Chile kufunga mikwaju yote mitatu ya mwanzo
ya penati huku Wareno wakikosa.
Shukrani kwa mlinda lango wa Chile Claudio Bravo ambaye aliokoa penati
tatu za Ricardo Quaresma, Moutinho na Nanj huku za Chile zikiwekwa
kambani na Vidal,Sanchez na Aranguiz.
Baada ya mchezo huo ambao Bravo anyeidaki Man City alikuwa mchezaji bora
wa mechi sasa Chile wanakwenda fainali wakisubiri mshindi kati ya
Ujerumani na Mexico kwa ajili ya fainali hiyo ya Confedaration Cup.
No comments:
Post a Comment