Meneja wa kiwanda cha TBL cha ilala,Calvin Martin akiwaelezea wageni mikakati ya kampuni kutumia nishati rafiki wa mazingira
Meneja wa Nishati na Maji wa TBL Group Peter Singisye (kulia) akifafanua jambo kwa ujumbe wa CTI na GIZ Sustainable Energy Programme ulipotembea kiwanda cha Ilala .Kutoka kushoto ni Mshauri wa matumizi bora ya nishati wa GIZ Consulting Group,Lydia Koch,Mraribu wa Matumizi ya Nishati wa shirikisho
la wenye viwanda Tanzania(CTI) Thomas Richard na Msimamizi Mkuu wa
matumizi bora ya nishati wa GIZ Sustainable Energy Programme ,Jesper
Vauvert.
Mtaalamu wa Mazingira wa Tbl Group, Coleta Mamburi (kulia) akifanua jambo kuhusiana na nishati
Meneja wa Afya na Usalama wa TBL Group ,Renatus Nyanda,akielezea masuala ya usalama kwa wageni hao walipotembelea kiwanda.
Wataalamu kutoka TBL Group katika picha ya pamoja na wageni wao baada ya kumalizika ziara
Wataalamu wa masuala ya nishati kutoka Shirika la maendeleo la Ujerumani (GIZ)
na Chama cha Wafanyabiashara wenye viwanda nchini (CTI) wamefanya ziara
katika kiwanda cha Tanzania Breweries jijini na kukutana na uongozi na
wataalamu mbalimbali wa masuala ya nishati ambapo pia walitembelea
sehemu mbalimbali za kiwanda na kujionea hatua mbalimbali za uzalishaji zinazofanyika kiwandani hapo.
Ziara
hilo ilikuwa na lengo la kujifunza mbinu inazotumia kampuni ya TBL
Group kupunguza matumizi ya nishati ya umeme kutoka gridi ya taifa
badala yake kubuni uzalishaji mbadala wa nishati ya umeme kutoka vyanzo
vingine ambayo tayari imeanza kutumika katika viwanda vilivyopo chini ya
kampuni hiyo.
Meneja wa kiwanda cha TBL cha ilala kilichopo jijini Dar es Salaam,Calvin Martin, aliwaeleza wataalamu hao kuwa
kampuni tayari imeanza kufanya uzalishaji kwa kutumia nishati ya umeme
wa jua katika kiwanda cha TBL cha Mbeya na nishati inayotokana na pumba
za mpunga katika kiwanda cha TBL Mwanza.
Calvin Martin aliwaeleza wataalamu hao kuwa matumizi
ya nishati hizo mbadala yameanza kuonyesha mafanikio kwa kupunguza
gharama za matumizi ya umeme wa kawaida ikiwemo kuwa rafiki wa
mazingira.
“Kampuni
inaendelea na mkakati wa kusambaza matumizi ya nishati hizi mbadala
katika viwanda vyake na kutumia vifaa vya uzalishaji vya teknolojia ya
kisasa lengo kubwa likiwa ni kupunguza matumizi ya gharama za umeme
katika uzalishaji na utunzaji wa mazingira.
Kutokana na ubunifu na jitihada hizi kampuni ya TBL Group mbali na kushinda Tuzo ya jumla ya Rais ya mzalishaji bora inayotolewa
na Chama cha wenye Viwanda Tanzania (CTI) pia ilishinda katika
kipengele cha matumizi mazuri ya nishati (Energy Efficiency Award.
No comments:
Post a Comment