KAMISHNA Msaidizi katika Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Simon Panga,
akizungumza kabla ya kukabidhi zawadi ya Idd El Fitri kwa niaba ya Rais
Dk. John Magufuli kwaVituo vya Yatima na Makundi Maalumu katika Maabusu
ya Watoto Dar es Salaam, leo.
KAMISHNA Panga, akikabidi zawadi
kwa Ofisa Ustawi wa Jamii Mfawidhi wa Makao ya Taifa ya Yatima
Kurasini, Dar es Salaam, Beatrice Mgumiro.
Picha Zote Na. Frank Shija.
Na. Lilian Lundo – MAELEZO
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli ametoa zawadi ya Idd El Fitri
zenye thamani ya shilingi 10,922,000 kwa vituo 9 vya Mkoa wa Dar es
Salaam, vituo 2 vya Zanzibar na vituo 13 kutoka mikoa ya Tanzania Bara.
Zawadi hizo zimekabidhiwa leo
katika Mahabusu ya Watoto iliyoko Upanga Jijini Dar es Salaam na
Kamishina Msaidizi wa Ustawi wa Jamii, Idara ya Ustawi wa Jamii, Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, na Watoto, Simon Panga kwa
niaba ya Mhe. Rais, Dkt. John Pombe Magufuli.
Panga amezitaja zawadi
zilizotolewa kuwa ni mchele, mbuzi na mafuta ya kupikia ambazo
zitawezesha makundi hayo kufurahi na kusherehekea sikukuu kama ilivyo
kwa watu wengi.
“Mhe. Rais kwa upendo wake wa
dhati kabisa ameona umuhimu wa kushiriki pamoja na watu walio katika
makundi maalum wakiwemo watoto walio katika mazingira hatarishi na
wazee wenye ulemavu wasiojiweza, wanaohudumiwa katika makazi, katika
kusherehekea sikukuu ya Idd El Fitri mwaka 2017,” amesema Panga.
Aidha, amevitaja vituo
vilivyonufaika na zawadi za Mhe. Rais kwa Mkoa wa Dar es Salaam ni Makao
ya Taifa ya Watoto Yatima Kurasini – Temeke, Makao ya Watoto IBN
Kathry- Ilala, Makao ya Watoto Yatima Msimbazi, Makao ya Watoto Yatima
Chakuwama, Makao ya Watoto Yatima Group Trust Fund – Temeke, Makao ya
Watoto Yatima Dar Al Arqum (International Islamic Relief Organization),
Mahabusu ya Watoto Dar es Salaam – Upanga, Makazi ya Wazee na Wasojiweza
Nunge – Kigamboni na Shule ya Ufundi ya Watoto Wenye Ulemavu Yombo.
Vile vile, amevitaja vituo
vilivyonufaika kwa upande wa mikoa ya Tanzania Bara kuwa ni Makao ya
Watoto Tosamaganga – Iringa, Makao ya Watoto Yatima Malaika Kids Home,
Mkuranga – Pwani, Makao ya Watoto Yatima Karibu Nyumbani, Kibaha –
Pwani, Makao ya Watoto Yatima Miyuji Cheshire – Dodoma, Shule ya
Maadilisho Irambo – Mbeya na Mahabusu ya Watoto – Mbeya.
Vituo vingine ni Mahabusu ya
Watoto – Arusha, Makao ya Wazee na Wasiojiweza Kolandoto – Sinyanga,
Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ngehe – Ruvuma, Makazi ya Wazee na
Wasiojiweza Kiilima – Bukoba, Kagera, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza
Magugu – Manyara, Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Ipuli – Tabora, Makazi
ya Wazee na Wasiojiweza Bukumbi – Mwanza.
Kwa upande wa Zanzibar, vituo
vilivyonufaika ni Kituo cha Watoto Yatima Mabaoni – Chakechake – Pemba
na Makazi ya Wazee na Wasiojiweza Sebleni – Unguja.
Utoaji wa zawadi hizo ni utaratibu
wa Waheshimiwa Marais tangu awamu nne zilizopita ambapo wamekuuwa
wakiwapatia makundi hayo maalum zawadi za vyakula katika sikukuu
mbalimbali.
No comments:
Post a Comment