Baraza la Michezo Tanzania (BMT),
limebariki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
likisema: “Tunaitakia TFF uchaguzi mwema wenye amani, upendo na
utulivu.”
Pamoja na baraka hizo, Baraza
limeiagiza TFF kuwaelekeza wagombea wote kuzipitia sheria za Baraza la
Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1)
na (2).
Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2),
inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa
sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa
mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali.
BMT imetoa agizo hilo ikiwa ni kukumbushana juu ya utii wa sheria na kuepuka kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja.
Katika barua yake iliyoandikwa
Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja,
Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini.
Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.”
Baraza limesisitiza kuwepo na haki
katika mchakato mzima kuelekea kwenye uchaguzi. Uchaguzi na mchakato
wake uwe huru na amani na usiwe ni kichocheo cha uvunjifu wa amani.
Baada ya viongozi kupatikana,
watakula kiapo cha utii, na kujaza fomu Namba 5 ya BMT ya utekelezaji
majukumu yao kama Kanuni ya 8 (4) inavyoeleza.
Kadhalika, mara baada ya uchaguzi,
Baraza limeagiza kuhusisha baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza ili
viendane na katiba za TFF na wadau pamoja na kanuni zao.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
No comments:
Post a Comment