Wednesday, 28 June 2017

Ujenzi wa jiwe la amri 10 za Mungu wapingwa

Wanaharakati katika jimbo la Arkansas nchini Marekani, wanapinga ujenzi wa jiwe moja kubwa lililo na maandishi ya amri 10 za Mungu, kwenye uwanja wa makao makuu ya bunge la jimbo hilo.
Wanasiasa walipitisha kauli ya ujenzi wa mnara huo wa jiwe wenye urefu wa futi sita, katika eneo la Little Rock mnamo mwaka wa 2015.
Muungano wa haki na uhuru wa raia nchini Marekani ACLU, umewasilisha kesi mahakamani kutaka kuondolewa mara moja kwa mnara huo, ukisema kuwa unaleta mgawanyiko na unakiuka ahadi ya uhuru wa kidini kwa wote, katika katiba ya Marekani.

Seneta wa chama tawala cha Republican, Jayson Rapert, ambaye alikuwa katika mstari wa mbele wa kutaka kuwekwa kwa jiwe hilo , alisema kuwa hatua hiyo inaenda sambamba na msimamo wa mahakama kuu ya Marekani, na hivyo ni jambo zuri kwa jimbo la Arkansas.

No comments:

Post a Comment