Tuesday, 27 June 2017

Donald Trump ametajwa kama Rais asiyekubalika zaidi Duniani:

 Rais Donald Trump wa Marekani ametajwa kama Rais asiyekubalika zaidi kuwahi kuchaguliwa na Taifa hilo takwimu zikionesha zaidi ya 80% ya wananchi hawampendi na zaidi ya 40% ya waliomchagua kujutia uamuzi wao, kwa mujibu wa Taasisi ya utafiti ya Pew Research Center.
Utafiti huo pia umeonesha Rais Trump ameisababishia Marekani kupoteza nguvu na ushawishi duniani ambapo zaidi ya nchi 37 zilizohusishwa kwenye utafiti huo ni nchi mbili pekee Urusi na Israel zilionesha kumkubali Rais huyo.
Sababu kubwa ziliyotajwa Trump kutokubalika ukilinganisha na mtangulizi wake Barack Obama ni sera yake ya kuwafukuza wahamiaji na kujenga ukuta kuitenganisha nchi yake na Mexico.
Aidha, Utafiti umeonesha kuwa Rais mstaafu Obama bado anakubalika kwa 90% Korea Kusini na Trump akikubalika kwa 10% huku Israel ikionekana kumkubali zaidi Trump kwa 56% na Obama akikubalika kwa 49%.



No comments:

Post a Comment