Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo (katikati) akisisitiza jambo wakati wa
ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na DAWASA.Kulia ni Kaimu
Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus Mwangi’ngo na kushoto ni Meneja wa
Kituo cha uzalishaji maji Ruvu Juu Bw. Emmanuel Makusa.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua miundo mbinu ya chanzo cha
maji ruvu juu wakati wa ziara yake ya kukagua miradi inayotekelezwa na
DAWASA.
Meneja wa Kituo cha uzalishaji
maji Ruvu Juu Bw. E. Mukasa (katikati)akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu
Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akikagua moja ya mitambo katika chanzo
cha maji ruvu juu,kulia ni Kaimu Mtendaji Mkuu wa DAWASA Romanus
Mwangi’ngo.
Sehemu ya miundo mbinu ya katika chanzo cha maji Ruvu juu.
Sehemu ya miundo mbinu ya katika chanzo cha maji Ruvu juu.
Katibu Mkuu Wizara ya Maji na
Umwagiliaji Prof. Kitila Mkumbo akioneshwa ramani ya mradi huo na hatua
iliyofikiwa katika ulazaji wa mabomba kutoka kwa meneja wa mradi huo
unaoanzia katika chanzo cha mto wami,mradi unaotekelezwa na Kampuni ya
WAPCOS ya India chini ya usimamizi wa DAWASA.
(Picha na Frank Mvungi-Maelezo)
Frank Mvungi-Maelezo
Serikali imesema imeridhishwa na
Utendaji kazi wa Mamalaka ya Maji Safi na Maji Taka (DAWASA) katika
kutekeleza miradi mikubwa ya maji kwa kuzingatia Sheria na Kanuni hali
inayoongeza tija katika mamlaka hiyo.
Akizungumza wakati wa ziara ya
kukagua miradi mbalimbali inayotekelezwa na DAWASA katika Mikoa ya Dar
es Salaam na Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Maji na Umwagiliaji Prof.
Kitila Mkumbo amesema moja ya miradi hiyo ni ule wa kupanua na kusambaza
maji katika mji wa Chalinze utakaonufaisha wakazi zaidi ya laki mbili.
“Kwa ujumla naridhishwa na kazi
inayofanywa na DAWASA katika kutekeleza miradi ya maji nawatia moyo
muendelee kufanya kazi hii kwa bidii ili azma ya Serikali kuwafikishia
wananchi huduma ya maji kwa wakati itimie” Alisisitiza Prof. Mkumbo.
Akifafanua Prof. Mkumbo amesema
katika ziara yake amejionea na kukagua miundo mbinu ya kusambaza
maji,ujenzi wa matanki ya kuhifadhi maji na miundo mbinu yote katika
chanzo cha maji Wami kinachopanuliwa ili kukidhi mahitaji ya wakazi wa
Chalinze .
“Wananchi wajenge utamaduni wa
kutunza rasilimali zilizopo ikiwemo miundo mbinu ya maji mbayo inajengwa
kwa gharama kubwa ili iweze kuwanufaisha Wananchi wote na kuchochea
maendeleo” Alisisitiza Prof. Mkumbo
Mradi mwingine uliotembelewa ni
ule wa uchimbaji visima vyenye urefu wa mita 600 kila kimoja vipatavyo
20 na kati ya hivyo 17 vimekamilika hivyo kuongeza upatikanaji wa maji
ambao utachochea maendeleo na ukuaji wa sekta ya Viwanda.
Visima hivyo vitawezesha
kuzalishwa kwa lita milioni 260 za maji kwa siku zitakazotumika katika
Wilaya ya Kigamboni na Jiji la Dar es Salaam.
Kwa upande wake Kaimu Mtendaji
Mkuu wa DAWASA mhandisi Romanus Mwangi’ngo amesema kuwa dhamira ya
Serikali ni kuhakikisha kuwa vyanzo vya maji Ruvu Juu na Ruvu Chini na
Visima vya Kimbiji na Mpera vitasaidia kufikisha kiwango cha maji
yanayozalishwa kufikia lita milioni 756 zitakazosaidia katika kuondoa
tatizo la maji katika Jiji la Dar es Salaam.
Aliongeza kuwa kwa upande wa
mradi wa Chalinze vituo vya kusambaza maji takribani 236 vimeshajengwa
kati ya 351 vilivyopangwa hali inayoonyesha kuwa mradi huo unaendelea
kutekelezwa kama ilivyopangwa na utakamilika mwezi oktoba 2017.
Ziara ya Katibu Mkuu Wizara ya
Maji na umwagiliaji kukagua miradi inayotelezwa na DAWASA katika mikoa
ya Dar es Salaam na Pwani imehusisha vyanzo vya maji vya Ruvu Juu,Mradi
wa uchimbaji Visima virefu Kimbiji na Mpera,Chanzo cha maji Wami
unakotekelezwa mradi mkubwa wa upanuzi na ulazaji mabomba, ujenzi wa
vituo vya kusambazia maji na matanki ya kuhifadhi maji Chalinze.
No comments:
Post a Comment