Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe(mwenye miwani) akisikiliza
maelekezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya
Michezo Bw. Alex Nkenyenge (wa Tatu kulia) alipotembelea uwanja wa
Taifa leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt.Harrison Mwakyembe (wa kwanza kushoto) akimsikiliza
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo wa Wizara hiyo Bw.
Alex Nkenyenge (katikati) alipokuwa akiwatambulisha vijana ambao ni
Maafisa kilimo (wenye makoti) leo Jijini Dar es Salaam , mwingine ni
Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba
Abbas(mwenye shati jeupe).
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kushoto) akipata maelekezo
kuhusu mbegu za nyasi mpya kutoka kwa Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw.
Julius Mgaya leo Jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea
uwanja huo.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) akionyeshwa mashine
zinazotumika katika ukarabati wa picth katika uwanja wa Taifa kutoka kwa
Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge
(aliyechuchumaa), katikati ni Meneja wa Uwanja wa Taifa Bw. Julius
Mgaya na kushoto ni Mkurugenzi wa Utawala na Utekelezaji kutoka
SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas leo Jijini Dar es Salaam .
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akielezwa jambo
kuhusu matumizi mashine ya kuchorea mistari kutoka kwa Meneja wa
Uwanja wa Taifa Bw. Julius Mgaya(aliyeinama) na kushoto ni Mkurugenzi
Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bw.Alex Nkenyenge leo Jijini
Dar es Salaam alipofanya ziara ya kutembelea uwanja huo. 9picha na
Lorietha Laurence WHUSM).
Na Lorietha Laurence WHUSM.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa
na Michezo Mhe.Dkt. Harrison Mwakyembe ameridhishwa na maendeleo ya
ukarabati wa eneo la kuchezea mpira (picth) la Uwanja wa Taifa wakati wa
ziara yake leo Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza katika ziara hiyo ya
kukagua hatua iliyofikiwa katika matengenezo ya uwanja huo Waziri
Mhe.Dkt. Mwakyembe amesema kuwa amefurahishwa na hatua ya awali ya
ukarabati na anatarajia mabadiliko makubwa zaidi baada ya hatua
zinazofuata kukamilika .
“Nimefurahishwa na mabadiliko
niliyoyaona katika hatua hii ya awali naamini ukarabati utakapokamilika
milango itakuwa wazi kwa mechi za kimataifa ikiwemo mashindano ya AFCON
yanayoratajiwa kufanyika nchini kwetu mwaka 2019” alisema Dkt.Mwakyembe
Aidha aliongeza kwa kusema kuwa
Serikali ipo katika mkakati wa kuhakikisha viwanja vingine vikiwemo vya
mikoani vinafanyiwa ukarabati ili kuboresha sekta ya michezo nchini.
Waziri Dkt. Mwakyembe ameushukuru
uongozi wa SPORTPESA kwa kuonyesha ushirikiano wa karibu na Serikali
katika kuhakikisha inaweka mchango wake katika michezo kwa kukarabati
sehemu ya kuchezea mpira (picth) ya Uwanja wa Taifa pamoja na vifaa
mbalimbali vilivyotolewa katika kuhakikisha kazi hiyo inakamilika.
Naye Mkurugenzi wa Utawala Na
Utekelezaji kutoka SPORTPESA Bw.Tarimba Abbas ameeleza kuwa kampuni yao
imefanya hivyo ikiwa ni njia ya kuonyesha uzalendo wa kupenda na
kuthamini vya nyumbani.
“Hatua hii ni ya awali baada ya
mechi ya Everton na Gorimahiya mnamo Julai 13 mwaka huu hatua
itakayofuata ni ya kuondoa nyasi zote na kuotesha mpya ambazo
zitachukuwa miezi mitatu kuwa sawa” alisema Bw.Tarimba.
Uwanja wa Taifa ulianza
matengenezo ya eneo la kucheze (pitch) rasmi katikati wa mwezi wa sita
lengo ni kuhakikisha nyasi zilizochakaa zinaondolewa na kuwekwa nyasi
mpya zitazodumu zaidi ya miaka 10 .
No comments:
Post a Comment