Wednesday, 21 June 2017

Uingereza imetoa msaada wa fedha sh Bil 28.6

LADI
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dk. Hassan Mshinda (kulia), akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mapema wiki hii, wakati serikali ya Uingereza ilipotangaza kuongeza ufadhili wake wa zaidi ya shilingi bilioni 28 katika miradi ya uvumbuzi na teknolojia hasa kwa watoto. Katikati ni Kiongozi wa Timu ya Uwekezaji kwa Watu ya Kitengo cha Kimataifa cha Maendeleo cha Uingereza (DFID) Tanzania, Getrude Kihunrwa na Kiongozi wa timu ya Mfuko wa kuendeleza Uvumbuzi  unaofanywa na mwanadamu (HDIF), David McGinty .  

Na Hellen David
Serikali ya Uingereza kupitia shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa
DFID, imetoa msaada wa fedha za Tanzania shilingi bilioni 28.6 kwa
ajili ya kusaidia uwekezaji kwenye miradi inayolenga
kuinua fursa katika ubunifu wa mambo kwa kutumia teknolojia mbalimbali.
Mradi huo umelenga hasa katika malezi bora ya watoto na Usafi wa Mazingira na niwa tatu kufanyika nchini ikiwa ni miongoni mwa miradi ambayo inatekelezwa kwenye ufadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Watu unaojulikana kama( HDIF) na Utasimamiwa na  Tume ya Sayansi  na Teknolojia (COSTECH ).
Akizungumza katika Uzinduzi huo Mkurugenzi wa (COSTECH) Dkt Hassan Mshinda alisema kuwa ni furaha kwa kuongezea fedha hizo kwani zitatoa nafasi nzuri kwa kupata Ubunifu wa vitu ambao utaleta maendeleo katika Nyanja ya afya pamoja na Elimu.
“Tunashukuru kwa kupata fedha hizi tena kwani nchi bado inahitaji sana kupata njia za kibunifu ambazo zitakuwa njia nzuri kwa kuweza  kumuelimisha mtoto ili baadae akikua awe na maendeleo mazuri Zaidi”Alisema Dkt Mshinda
Aidha Dkt Mshinda alisema kuwa utafiti waliofanya wao unaonyesha kuwa Mtoto akiwa tumboni na hata baada ya kuzaliwa ni rahisi kumfundisha na akashika jambo vizuri na lisimtoke hata akiwa mkubwa.
“Utafiti Unaonyesha kuwa ili mtoto afanye Vizuri Ukubwani Maendeleo yao yanaanza tangu akiwa mdogo kabisa nando wakati Ubongo wao unaanza kukua pamoja na njia zao za fahamu zinakua ambapo kuna uhusiano mkubwa sana mtu anayefanya vizuri kimaisha na namna alivyoweza kulelewa toka akiwa mtoto mchanga kabisa”.Aliongezea Dkt Mshinda
Kwa upande wake Mkuu wa kitengo kinachosimamia masuala ya uwekezaji wa DFID Bi.Getrude Mapunda alizungumzia namna fedha hizo zitakavyosaidia kuinua  maendeleo katika sekta hiyo ya elimu pamoja na Upande wa Mazingira.
“Tumekuwa tukitoa fedha katika Mradi huu wa Ubunifu toka Mwaka 2014 kwa kushirikiana karibu sana na COSTECH ambapo hadi sasa tumepata mafanikio makubwa katika miradi iliyopita 36 imeshafanikiwa na awamu hii ya tatu tunaelekeza sana katika usafi wa mazingira ,hedhi kwa wasichana pamoja na makuzi ya watoto wadogo  kuanzia miaka sifuri hadi miaka 5”
Naye Mwakilishi Mkazi wa HDIF Bw. David MacGinty alieleza kuwa kutokana na mafanikio yaliyopatikana kwenye miradi iliyopita ndiyo maana wameona ipo haja ya kuongeza ufadhili katika awamu hii ya tatu.

HDIF ilizinduliwa Mei 2014 na Makamu wa Rais Mstaafu awamu ya nne Dk Mohamed Gharib Bilal  ambapo lengo lao la kuanzisha ni  kuongeza kasi ya maendeleo pamoja na  matumizi ya sayansi na teknolojia katika maendeleo.

No comments:

Post a Comment