Mchungaji wa Kanisa la Maombezi (GRC), Anthony Lusekelo alimaarufu kama
'Mzee wa Upako' amefunguka na kusema mtu kufa maskini si jambo la
kusifiwa hata kidogo kuwa ni uzalendo bali ni Ufala.
Mchungaji Lusekelo amesema hayo alipokuwa akiongea na mtangazaji wa kipindi cha UJENZI cha EATV kinachoruka kila Jumapili.
Mzee wa Upako anasema mtu anapokufa akiwa ameacha mali za kutosha ni
jambo jema kwani familia yake nyuma haiwezi kupata taabu wala watoto
hawawezi kupata shida tofauti na yule anayekufa akiwa na kitanda tu
kwani watoto wake watapata shida na mateso.
"Watu wanamsifu mtu amekufa bila mali eti alikuwa mwadilifu yaani
unakuta mtu amefanya kazi serikalini miaka na miaka, sijui miaka 35 au
40 anakufa hata kitanda hana.
"Wapo watu wanasema huyu jamaa alikuwa mzalendo na muadilifu sana hata
kitanda hana, hamna mtu huyo alikuwa fala umenielewa?, huyu alikuwa fala
na hastaili kuwa kielelezo cha msingi tuhoji mtu kapata mali wapi?
"Ndio jambo la msingi sababu unaacha watoto duniani unadhani wataishi
vipi? Mama anakuwa na nyumba pale anachota kodi anapeleka watoto shule
maisha yanaendelea" alisisitiza Mzee wa Upako.
No comments:
Post a Comment