Makamu wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Nyamlani aliwasilisha barua TFF
leo Jumapili Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya
Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania
nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni masuala binafsi.
Kwa msingi huo, wagombea
wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili
kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais wa sasa, Jamal
Malinzi anayetetea nafasi.
Mbali ya Malinzi wengine
wanaowania nafasi hiyo ni Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa,
Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na
Emmanuel Kimbe.
Waliojitokeza kuwania Makamu wa
Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey
Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa.
Mbali ya nafasi za urais na
makamu rais, Abdallah Mussa – aliyekuwa akiwania nafasi ya kugombea
ujumbe wa Kamati ya Utendaji TFF kutoka Kanda Na. 1 (Mikoa ya Kagera na
Geita) aliondolewa kwa sababu ya kutoambatanisha kivuli cha cheti ya
elimu ya sekondari.
Hivyo wagombea wa nafasi za Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:
Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;
- Soloum Chama
- Kaliro Samson
- Leopold Mukebezi
Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;
- Vedastus Lufano
- Ephraim Majinge
- Samwel Daniel
- Aaron Nyanda
Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;
- Benista Rugora
- Mbasha Matutu
- Stanslaus Nyongo
Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;
Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;
- John Kadutu
- Issa Bukuku
- Abubakar Zebo
- Francis Michael
Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;
- Kenneth Pesambili
- Baraka Mazengo
Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;
- Elias Mwanjala
- Cyprian Kuyava
- Erick Ambakisye
- Abousuphyan Silliah
Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;
- James Mhagama
- Golden Sanga
- Vicent Majili
- Yono Kevela
Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;
- Athuman Kambi
- Dunstan Mkundi
Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;
- Hussein Mwamba
- Mohamed Aden
- Musa Sima
- Stewart Masima
- Ally Suru
- George Benedict
Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;
- Charles Mwakambaya
- Gabriel Makwawe
- Francis Ndulane
- Hassan Othman ‘Hassanol’
Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga
- Khalid Mohamed
- Goodluck Moshi
- Thabit Kandoro
Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam
- Emmanuel Ashery
- Ayoub Nyenzi
- Saleh Alawi
- Shaffih Dauda
- Abdul Sauko
- Peter Mhinzi
- Ally Kamtande
- Said Tully
- Mussa Kisoky
- Lameck Nyambaya
- Ramadhani Nassib
- Aziz Khalfan
- Jamhuri Kihwelo
- Saad Kawemba
- Bakari Malima
No comments:
Post a Comment