Amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumo wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki.
“Mimi nina mitandao yote ya simu, nina Tigo, Airtel, Vodacom na hata TTCL, mtu akinitafuta huku Airtel,akanikosa ninaweza kuweka Tigo, ili mradi ninatambulika kila mahali,” amesema
Pia amesema, mitandao hiyo ya simu inamsaidia kupata taarifa mbalimbali zinazoendelea nchini na duniani.
Hata hivyo, Rais amezitaka kampuni za simu kuhakikisha zinalipa kodi ili serikali isikose mapato yake.
Pia Rais amesema hataki kuona taasisi nyingine zinajenga vituo vya ukusanyaji taarifa (Data centre)na badala yake fedha hizo zitumike kwa ajili ya shughuli nyingine za maendeleo.
“Data Centre kama hii ni mkombozi mwingine wa kupunguza kero mbalimbali, kwa sababu ukijaza vocha yako uko Zanzibar, ukinunulia vocha yako Kigoma au Moshi, hiyo pesa inakuja TRA, hakuna mabishano” amesema
Rais amesema hayo leo Juni Mosi, wakati wa uzinduzi wa mfumowa wa serikali wa ulipaji kodi kwa njia ya kielektroniki ambako pia alitembelea kituo hicho cha ukusanyaji taarifa.
Amesema chombo hicho kina faida yake na hivyo akawaomba watanzania, wawekezaji na wafanyabiashara kukitumia chombo hicho kwa manufaa ya taifa zima.
No comments:
Post a Comment