Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
(Kushoto) akiwa ameongozana na Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda na
Mkewe Tunu Pinda walipo mpokea katika makazi yao yaliyopo Zuzu Nnje
Kidogo ya Mjini Dodoma June 17, 2017 kuhudhuria Misa ya kumbukumbu
ya Marehemu Mzee Exavery Pinda Baba Mzazi wa Mizengo Pinda, Pamoja
nakuongoza Uchangiaji wa Ujenzi wa Nyumba ya Paroko na Ukarabati
wa Kanisa la Parokia ya ZUZU
Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
kwaniaba ya familia yake akimkabidhi Mchango wa Shilingi Milioni Kumi
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo Pinda . Kwa ajili ya kuchangia ujenzi
wa Nyumba ya Paroko pamoja nakufanyia Ukarabati wa Kanisa Parokia
ya ZUZU Dodoma, Kushoto ni Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba
Chesco Msaga . Harambe hiyo imefanyika June 17, 2017 katika Makazi
ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya Mjini
Dodoma
Waziri Mkuu Mstaafu Mizengo
Pinda akiwaonyesha Wageni waalikwa Shilingi Milioni Kumi Mchango alizo
kabidhiwa na Wziri Mkuu Kassimu Majaliwa kwa niaba ya Familia yake ,
Kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa Nyumba ya Paroko pamoja nakufanyia
Ukarabati wa Kanisa Parokia ya Zinje (ZUZU)Dodoma, Kushoto ni
Msaidizi wa Askofu Jimbo la Dodoma Baba Chesco Msaga . Harambe hiyo
imefanyika June 17, 2017 katika Makazi ya Waziri Mkuu Mstaafu Pinda
yaliyopo ZUZU Nnje kidogo ya mjini Dodoma
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
amesema wazazi wana jukumu la kulea watoto kwenye misingi ya kumcha
Mungu ili Taifa liweze kuwa na watu waadilifu na wachapakazi.
“Taifa la watu waadilifu na
wachapakazi huanzia katika ngazi ya familia. Kama kaya zetu haziishi kwa
uadilifu, ni vigumu sana kuwa na Taifa lenye wananchi waadilifu. Ni
muhimu basi familia zetu zihakikishe kuwa tunakuwa na watoto wenye hofu
ya Mungu na wenye kumcha Mungu,” alisema.
Alitoa kauli hiyo jana (Jumamosi,
Juni 17, 2017) wakati akizungumza na wageni waliohudhuria harambee ya
kuchangia ujenzi wa kanisa na nyumba ya Paroko katika Parokia Teule ya
Zuzu, nje kidogo ya mji wa Dodoma.
Harambee hiyo ilitanguliwa na
ibada ya misa ya shukrani kwa ajili ya marehemu Mzee Xavery Mizengo
Pinda, ambaye ni baba yake, Waziri Mkuu mstaafu, Mizengo Peter Pinda.
Mzee Xavery Pinda alifariki Novemba 27, mwaka jana katika hospitali ya
mkoa wa Dodoma na kuzikwa kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele,
Katavi.
Waziri Mkuu alisema wazazi
wanapaswa kujitathmini juu ya malezi ya watoto wao na kujihoji kama
wamepata malezi yanayostahili. “Kupitia funzo tulilolipata leo,
tujitathmini kuhusu makuzi ya watoto wetu. Je watoto wetu wanapata
malezi stahiki? Je tunawalea katika misingi ya kutoa kwa ajili ya Mungu
au tunawafundisha wajilimbikizie mali? Je, tunawahoji watoto wetu kuhusu
utajiri wanaoupata ghafla? Au tunawapongeza na kufurahia bila kujua
wanapata wapi utajiri huo?,” alihoji.
“Nitumie nafasi hii kuwasihi
wazazi wote kwamba tujitahidi kuwekeza katika malezi ya watoto wetu. Ili
tuwe kioo cha aina ya Taifa tunalotaka kulijenga, hatuna budi kuwalea
watoto wetu katika misingi ya imani, uadilifu na uzalendo mkubwa kwa
nchi yetu,” alisisitiza.
Katika harambee hiyo, Waziri Mkuu
na mke wake walichangia sh. milioni 10 ambapo jumla ya sh. milioni 160
zilikusanywa. Kati ya hizo, sh. 111,150,000 zilikuwa ni ahadi, sh.
38,447,000 zilikuwa ni fedha taslimu na sh. 10,403,000 zilikuwa ni vifaa
vya ujenzi.
Mapema, akiongoza ibada ya
shukrani, Makamu wa Askofu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dodoma, Padre Chesco
Msaga alisema kila mtu anapaswa kumshukuru Mungu kwani hakuna mwanadamu
anayeweza kudai kuwa yuko jinsi alivyo kwa sababu ya akili zake.
“Hata sisi tunasahau kumshukuru
Mungu hasa pale mambo yetu yanapotunyookea. Tunadhani ni kwa akili zetu
ndiyo mambo yetu yananyooka. Tunapaswa tukumbuke kuwa maishayetu yapo
mikononi mwa Mungu, na yeye ndiye anajua njia zetu,” alisema akirejea
mfano wa wakoma 10 walioponywa na Bwana Yesu na mmoja tu ndiye alirudi
kushukuru.
Kwa upande wake, Waziri Mkuu
mstaafu, Mizengo Pinda alisema harambee hiyo inafuatia uamuzi wa Askofu
Mkuu wa Jimbo Kuu la Dodoma, Mhashamu Beatus Kinyaiya wa kuiteua Zuzu
iwe parokia.
“Sasa hivi tulikuwa na kigango.
Kuteuliwa kuwa parokia maana yake tutakuwa na padre anakaa hapa Zuzu saa
24 na tutakuwa na ibada kila Jumapili, na katikati ya wiki kadri ratiba
zitakavyoruhusu.
“Kikubwa tunachopaswa kufanya
kufuatia uamuzi huo, ni kuhakikisha kuwa mapadre wana nyumba ya kuishi.
Sasa hivi, wa kwetu anakaa Dodoma mjini. Kwa hiyo tuna kazi ya
kukarabati kanisa, lakini kwanza tukamilishe ujenzi wa nyumba ya
mapadri,” alisema wakati akielezea madhumuni ya harambee hiyo.
No comments:
Post a Comment