Serikali ya Cuba imelaani vikali hatua ya Rais Trump kuiwekea upya vikwazo vya usafiri na biashara taifa hilo baada ya utawala wa Barak Obama kulegeza sheria hiyo, katika harakati ya kuboresha uhusiano baina ya mataifa hayo mawili.
Akiwahutubia wamarekani wenye asili ya Cuba mjini Miami, Trump amesema
hatua yake imechangiwa na rekodi ya Cuba ya Ukiukaji wa haki za binadamu
hasa, wakati wa utawala wa kidikteta wa Fidel Castro.
Amesema sera hiyo mpya itatilia mkazo sheria juu ya usafiri na kutuma fedha nchini humo.
Havana hata hivyo imeskitishwa na uamuzi huo na kuongeza kuwa unarudisha
nyuma ushirikiano wa kimaendeleo baina ya mataifa hayo na kwamba
Marekani haiwezi kuishauri Cuba juu ya masuala ya haki za binadamu.
No comments:
Post a Comment