Sunday, 18 June 2017

Fifa yajipanga kujadili Pendekezo la kupunguza dakika 90 za mechi

Shirikisho linaloweka sheria za soka duniani lina mpango wa kupunguza muda wa kipindi cha kwanza na kile cha pili cha mchezo ili kuwa dakika 30.
Bodi ya kimataifa ya soka duniani itajadili pendekezo hilo linalolenga kupoteza muda unaopotezwa kwa makusudi.
Waliopendekeza mpango huo wanasema kuwa mechi huchezwa kwa dakika 60 pekee kati ya tisini na muda uliosalia hutumiwa kupoteza wakati.
Wanapendekeza dakika 30 kila kipindi huku muda ukisimamishwa kila mpira unapotoka kusaidia kukabiliana na muda unaopotezwa mbali na kuufanya mchezo kuvutia zaidi.
Wakosaoji wanasema kuwa mabadiliko kama hayo hayatakuwa na umuhimu wowote iwapo sheria ya kupoteza muda itaimarishwa.
Pendekezo jingine litasababisha wachezaji kutoruhusiwa kupiga mpira mara ya pili baada ya kipa kuupangua wakati wa penalti.
Na iwapo penalti hiyo haikupigwa ilivyotarajiwa ,mchezo utasitishwa na mpira wa adhabu kutolewa.
Mapendekezo mengine yanashirikisha kuweka saa katika uwanja ambayo italingana na ile ya refa mbali na sheria mpya itakayoruhusu mchezaji kujipigia mpira ama hata kutamba na mpira wakati anapopiga mpira wa adhabu.

Tayari aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Gianfranco Zola anapendelea pendekezo hilo la kupunguza muda wa dakika za mechi hadi 60.

No comments:

Post a Comment