Thursday, 8 December 2016

RC Gambo kukabidhi Pikipiki 200 – Jumamosi.

sar1
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizungumza na waendesha boda boda 200(hawapo pichani) watakaopatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba wakati wa kikao na vijana hao kukamilisha taratibu na masuala ya usalama kabla ya kukabidhiwa Pikipiki hizo.
sar2Kijana muendesha boda boda(aliyesimama) akichangia kuhusiana na kiasi gani cha Fedha kirejeshwe kwa siku ili kukamilisha mkopo wa Pikipiki watakazopewa. Kwa wakati.
sar3Umoja wa waendesha bodaboda Jiji la Arusha (UBOJA) wakiwa katika Kikao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
sar4
 Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkubwa akitoa maelezo ya mafunzo ya udereva yatakayotolewa bure kwa vijana hao kuanzia tarehe 08/12/2016 kwenye Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

Nteghenjwa Hosseah, Arusha.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo mapema leo amekutana wa waendesha boda boda 200 watakaonufaika na mradi wa kuwainua vijana kiuchumi katika Jiji la Arusha kwa kupatiwa Pikipiki zisizokuwa na riba.
Mhe. Gambo amekutana na vijana hao ili kukamilisha taratibu za mwisho na kuangalia masuala ya usalama kabla hawajakabidhiwa Pikipiki hizo.
Katika Kikao hicho vijana hao wamekubalina kwa Pamoja kwamba watarejesha Tsh 7,000 kwa siku na pia na kwa atakayeweza kwa wiki Tsh 49,000 ama kwa Mwezi itakua Tsh210,000.
Pia walikubaliana kwamba ni ruksa kwa yeyote atakayeweza kulipia zaidi ya kiasi icho ili aweze kumaliza mkopo wa Pikipiki yake na aweze kumilikshwa Pikipiki hiyo.
Haikatazwi kwa mtu yeyote kuleta zaidi ya Tsh 7,000 kwa siku ili uweze kumalizia mkopo wako mapema na ikitokea  umekamilisha  mkopo huo hata kwa  miezi miwili unamilikishwa  Pikipiki alisema Mhe. Gambo.
Vijana hao pia walihoji kuhusu service ya Pikipiki hizo na Mwakilishi wa Kishen Enterprises Ltd ambao pia ni mawakala wa Pikipiki aina ya Toyo Mkoani hapa alisema Pikipiki hizo zina warrant wa meizi sita na endapo zitapata hitilafu kwenye Engine katika kipindi hicho wataweza kuifanyia matengenezo bila gharama yeyote au kubadilishiwa Pikipiki nyingine.
Kwa hesabu za kawaida vijana hawa watarejesha Tsh 2,135,000 kwa mchanganuo ufuatao:
Tsh 2,000,000 ni Bei ya Pikipiki
Tsh 135,700 ni gharama ya Bima Kubwa hivyo
Vijana hao watarejesha Tsh 7,000 X siku 305 = 2,135,000.
Tunaposema watalipia kwa kipindi cha mwaka mzima tunaamisha siku 60 zitakua kwa ajili ya service na dharura nyingine na siku 305 ndio watakazoleta marejesho Alimalizia Mkuu wa Mkoa.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha amesema Pikipiki hizo zitakabidhiwa siku ya Jumamosi tarehe 10/12/2016 saa nne Asubuhi kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.

No comments:

Post a Comment