Na Immaculate Makilika –MAELEZO
Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu Mstaafu
wa Chama cha Mapinduzi na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Yusuph Makamba
alisema kuwa Rais Magufuli anafanana na Yohana Mbatizaji kwa vile ni
kiongozi anayefanyakazi bila kuogopa.
Makamba ametoa kauli hiyo leo kwa njia ya simu katika mahojiano maalum na Mwandishi wa habari hizi.
Makamba alisema kuwa Rais ni
kiongozi mchapakazi ambaye hayumbushwi na maneno wala vitisho kwa vile
anasema ukweli katika kutekeleza majukumu yake.
“Yohana Mbatizaji alisema ukweli
na hakutikiswa na upepo, hakuogopa macho ya watu wala hakuwa mtu wa
majigambo, kama ilivyoandikwa katika Biblia Takatifu Marko 6:12, na
hivyo ndiyo navyomfananisha Rais wetu Magufuli na viongozi wote tumuunge
mkono” alisema Makamba.
Aidha, kuhusu maika 55 ya Uhuru ,
alisema kuwa ni vyema Watanzania wakazingatia wito wa uhuru ni kazi, na
kwa kuwa Serikali hii imeweka mkazo katika ufanyaji kazi.
Makamba alisema kuwa katika Awamu
hii ya HAPAKAZI TU, inaakisi wito wa Uhuru katika vipindi mbalimbali
kuanzia kipindi cha Uhuru ni kazi na Uhuru na kazi mara baada ya
kupatikana kwa Uhuru na kuwakumbusha watanzania kuulinda Uhuru.
“Ni lazima kuulinda Uhuru kwa
gharama yeyote ili amani na mshikamano uendelee kuwepo basi hatuna budii
kuepuka lugha zenye maneno ya uchochezi, ukabila na udini” alisema
Makamba
No comments:
Post a Comment