Rais Dkt John Magufuli amezirudisha nyumba zote zilizohamishwa kutoka shirika la nyumba NHC kwenda ofisi ya Rais tawala za mikoa na serikali za mitaa TAMISEMI katika mikoa 20.
Akitoa malalamiko yaliyotolewa June 22 mwaka huu na wakazi 644 wa Magomeni Kota, Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi, William Lukuvi alisema, “Rais Magufuli ameagiza kuwa mkataba wa kujengea nyumba wakazi hao ambao Manispaa ya Kinondoni umeshindwa kutekeleza na kwa sasa mkataba huo utatekelezwa na serikali kupitia wizara yake.
Amesema wazee wote wanaoishi katika nyumba hizo zilizohamishwa kutoka shirika la nyumba NHC kwenda TAMISEMI kuwa wasihamishwe hadi utaratibu mpya utakapotolewa na serikali na kuwataka wazee hao kuendelea kulipa kodi kama kawaida.
“Kwahiyo mheshimiwa Rais amefanya uamuzi mwingine kwamba nyumba zote zilizohamishwa mwanzo mwaka 1990 za National Housing kuja TAMISEMI sasa zirudi serikali kuu. Kwahiyo nyumba kama Magomeni na zote zilizopo mikoa 20 yote Tanzania zimehamishwa sasa zitasimamiwa na serikali kuu, ardhi na nyumba zake,” alisema Lukuvi.
Baadhi ya wakazi wa Magomeni wameishukuru serikali kwa uamuzi huo wakiiomba kulishughulikia suala hilo kwa haraka kwani manispaa ya Kinondoni imewazungusha tangu mwaka 2011 nyumba zao zilipovunjwa katika eneo hilo.
Waliongeza kwa kusema lile eneo walilotuvunjia sasa hivi wanapaki magari, wa mwisho alimalizia kwa kusema, “tunaomba serikali itusaidie isionyeshe ubabaishaji kama uliofanyika pale manispaa.”
No comments:
Post a Comment