Tuesday, 2 August 2016

Picha za Mastaa wenye followers wengi kwenye mitandao ya kijamii Tanzania

Picha ya pamoja ya mastaa takriban 40 waliosanishwa na Binary By Aggrey & Clifford
 Kwa muda mrefu sasa wasanii wenye followers wengi kwenye mitandao ya kijamii nchini wamekuwa wakiingiza fedha kutoka kwa watu na makampuni yanayotaka kutangaza biashara kwenye akaunti zao lakini hakukuwa na utaratibu rasmi na bei zilizopangwa kiutaalamu.

Chege, Feza Kessy na Ommy Dimpoz
 Na sasa kampuni ya matangazo nchini, Aggrey & Clifford imezindua app maalum kwaajili ya kusimamia matangazo ya kwenye mitandao ya kijamii ikihusisha mastaa wenye ushawishi zaidi Tanzania.
AY ni mmoja wa mastaa 40 waliosainishwa
 App hiyo iitwayo Binary, imezinduliwa jana kwenye hoteli ya Hyatt Regency na kuhudhuriwa na mastaa takriban 40 wa kwanza waliosanishwa kwenye app hiyo.

Akiongea kwenye uzinduzi huyo, Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Aggrey & Clifford, Rashid Tenga alisema kuwa waliamua kutengeneza application ya simu itakayoweza kupandisha matangazo kwenye akaunti za mitandao ya kijamii za mastaa waliosaini mkataba bila wao kuhangaika kuyaweka.


 

Feza Kessy: Kupost vitu kwenye mitandao ya kijamii kumegeuka kuwa ajira
 Tofauti na njia ya kawaida ya kuweka matangazo hayo, app ya Binary inawawezesha kujua ni muda upi watu wanasoma zaidi matangazo (prime time) na hivyo kuwekwa katika muda muafaka.

Pia walitengeneza gharama husika (rate card) kwa kuzingatia wingi wa followers alionao staa husika. Alidai kuwa hadi sasa wamesaini mastaa 40 wanaowapa uhakika wa kuwafikia watu zaidi ya milioni 30
.
 “Hiyo ni zaidi ya jinsi gazeti linavyoweza kukupa, TV yoyote, na redio yoyote,” alisisitiza Tenga.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Maendeleo ya Biashara wa Binary by Aggrey & Clifford, Eni Kihedu alisema kuwa kwa utafiti waliofanya, matangazo kwa njia ya mitandao ya kijamii yanafikia watu wengi kwa asilimia 1000 zaidi ya njia za kawaida.

“Ukicompare digital media houses ambayo ni kutangaza kupitia social media houses ukiweka post zako 10 kwa kila mtu, kwa mwezi kama wanavyofanya kwenye magazeti ni over a thousand percent tangazo lako linaonekana kuliko kwenye tradional print media na hiyo ni the same kwa radio na TV,” alisema Ms
Kihedu.
 Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel ambaye aliisifia kampuni ya Aggrey & Clifford kwa kuanzisha utaratibu huo utakaokuwa na manufaa makubwa kiuchumi kwa mastaa wa Tanzani.
 Akiwaita jukwaani Diamond, Mwana FA na Wema Sepetu na Jacqueline Wolper kwa nyakati tofauti, Prof. Ole Gabriel aliwaeleza jinsi ambavyo umaarufu wao umewatengenezea brand itakayowalipwa na kwamba inapaswa ilindwe kwa namna yoyote ile.

“Kinachofanyika hapa ni kuhakikisha kwamba huo umaarufu wako uwe branded,” alimweleza Diamond. “Endelea kuutunza na Mungu akusaidie ili wanao na wajukuu zako nao wafaidi umaarufu wako.”

Mwenyekiti Mtendaji wa kampuni ya Aggrey & Clifford, Rashid Tenga akiongea kwenye uzinduzi huo
 Alisema kuwa serikali imefuruhishwa na ujio wa Binary na kuiomba kampuni hiyo kuhakikisha hakuna msanii anayedhulumiwa haki yake kwenye biashara hiyo.

Pia aliyaomba makampuni mbalimbali kutambua kuwa matumizi ya mitandao ya kijamii yamekuwa muhimu kiasi ambacho haipukiki kupeleka matangazo huko.

 Aliipongeza kampuni hiyo kwa kuangalia fursa za kimtandao na kuanzisha kitu ambacho kitawainua wasanii wengi kiuchumi huku pia serikali ikiingiza kodi.

Akizungumza kwa niaba ya wasanii wenzake, Diamond alisema ni muda wa wasanii kuanza kuitumia vizuri mitandao ya kijamii ili kuyavutia makampuni kama hayo kuwaamini na kuwatumia.

“Ni vizuri kuitumia kwa nafasi nzuri ili hata hawa wakiweka ujumbe labda matangazo ya kampuni zingine basi ifike kwa namna nzuri,” alisema Diamond.

Vigezo vilivyotumika kuwachukua mastaa hao wa kwanza ni ushawishi walionao, nguvu ya wanachokiweka kwenye mitandao ya kijamii na mrejesho unaopata (engagement) na wale ambao wamekuwa wakizitumia akaunti zao kwa maadili yanayotakiwa.

 Tazama picha zaidi za uzinduzi huo.






 Katibu Mkuu Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo, Prof Elisante Ole Gabriel akiwa na CEO wa Aggrey & Clifford, Rashid Tenga



No comments:

Post a Comment