Mkuu
wa wilaya ya Kibaha ,Assumpter Mshama,akizungumza na walimu wakuu wa
shule za Msingi wilayani humo ambapo alitoa maagizo mbalimbali ikiwemo
kuacha kuwalinda walimu wasio na maadili kazini.Mkuu huyo anaendelea na
zoezi la kukutana na makundi mbalimbali. (Picha na Mwamvua Mwinyi)
Na Mwamvua Mwinyi, Kibaha
MKUU wa wilaya ya
Kibaha ,Assumpter Mshama ,ametoa rai kwa walimu wakuu wa shule za msingi
wilayani humo, kuwafichua walimu walevi kazini na watoro pasipo
kuwalinda ili kulinda nidhamu kazini.
Amesema wapo baadhi ya walimu wanaoshindwa kufuata maadili yao ya kazi ambapo hakuna hatua zinazochukuliwa.
Aidha Assumpter amewataka walimu hao wakuu kuacha kuwaonea haya walimu hao wanaoshindwa kutimiza wajibu wao wa kazi.
Alitoa rai hiyo ,wakati
alipokuwa anazungumza na walimu wakuu wa shule za msingi wilayani hapa
,katika ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya.
Assumpter aliwaomba
wasikubali kukalia tabia hizo ikiwemo kulewa wakati wa kazi kwani kwa
walimu wataoshindwa kuwachukulia hatua wanaojihusisha na ulevi,utoro
wanaweza kujiweka katika mazingira magumu ya kazi.
Aliwaasa walimu kufanya kazi kwa wito, ari na molari ya kazi ili kuinua kiwango cha taaluma wilayani Kibaha.
“Kufanya vibaya kwa
baadhi ya shule ,kunasababishwa na changamoto mbalimbali ikiwemo walimu
kujiingiza na vitendo vya ulevi na utoro,wanakuwa kikwazo katika
kuendeleza sekta hii muhimu”
“Walimu wakuu msikubali
kuwafumbia macho walimu wa aina hiyo kwani kama mnavyosikia ngazi za
juu wanavyowatumbua, huku nako wasipokuwa makini tusiwafumbie macho,”
alisema Assumpter.
Nae afisa taaluma
halmadhauri ya wilaya hiyo, Damas Kimaro alielezea changamoto ambazo
zinasababisha kushuka katika ufaulu kitaifa kutoka nafasi ya 4 mpaka ya 9
imechangiwa na mchakato wa uchaguzi mkuu uliomalizika.
Mwalimu Uhai Legeza
,alimtaka mkuu huyo atembelee katika shule mbalimbali ili aweze kujionea
namna walimu hao wanavyofanyakazi katika mazingira magumu .
Alisema kuwa baadhi ya
walimu hukaa katika ofisi ambazo hazina thamani bora ikiwemo viti na
meza wanazotumia hazilingani na nyingi hazina ubora.
“Mkuu tembelea katika shule zetu uone viti na meza tunazotumia katika kutimiza majukumu yetu ya kazi,” alisema Legeza.
Kufuatia ombi hilo Assumpter aliahidi kutembelea shule hizo kujionea hali hiyo .
Anasema baada ya
serikali kumaliza tatizo la madawati sasa itageukia uboreshaji wa
miundombinu ya majengo ili kuhakikisha sekta ya elimu inaboreka zaidi.
No comments:
Post a Comment