Wachezaji wa Mbeya City.
Mchezo huo unatarajia kuwa mkali kwani kila timu itawatumia vijana waliowasajili huku Prisons ikiwa na kocha mpya, Abdul Mingange, ambaye aliifundisha Mbeya City msimu uliopita.
Katibu wa Mrefa, Seleman Haroub alisema chama chake kimeandaa michezo hiyo ili wananchi wazione timu zao zilivyojiandaa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu na zile za Daraja la Kwanza.
Alisema timu nyingine zitakazoshiriki mashindano hayo ni za Mbeya Kwanza ya mkoani hapa, Kimondo kutoka Songwe na Njombe Mji ya mkoani Njombe, zote Daraja la Kwanza.
“Mashindano haya yanaanza Jumatano kwa kuzikutanisha Tanzania Prisons na Mbeya Kwanza na lengo letu ni kuona timu hizi zilivyojiandaa kwa ligi zao zinazotarajia kuanza hivi karibuni,” alisema.
“Tulitamani kuona timu zote za Kanda za Nyanda za Juu Kusini zinazoshiriki Ligi Kuu na Daraja la Kwanza zinacheza mashindano haya, lakini baadhi hazitakuwapo kutokana na sababu mbalimbali,” alisema Haroub.
Aliitaja timu ya Majimaji ya Ruvuma, ambayo alisema ilipewa mwaliko, lakini imeshindwa kutokana na sababu zisizozuilika.
Katibu huyo alisema mashindano hayo yanatarajia kumalizika Agosti 11 na baada ya hapo watakutana na wadau pamoja na viongozi wa timu ili kuweka mikakati ya timu zao kufanya vizuri kwenye ligi.
No comments:
Post a Comment