Tuesday, 31 October 2017

MAGAZETI YA LEO JUMATANO NOV O1 2017




Milioni 50 zimekwama kutolewa kila kijiji kutokana na huduma za jamii kutokuwa vizuri

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, ameeleza sababu zinazomfanya achelewe kutimiza ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji alizoziajidi wakati wa kampeni za kugombea urais kuwa ni kutokana na kuwepo kwa mambo mengi nchini yanayohitaji utekelezaji wa haraka.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa Mkoa wa Mwanza katika mkutano wa hadhara ikiwa ni moja ya vitu alivyopanga kuvifanya katika ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani hapo.
Ameeleza kuwa ameona ni sahihi kuanza na mambo ya muhimu zaidi kama vile miundombinu ya barabara, huduma za afya pamoja na elimu kabla ya kutoa fedha hizo ambazo aliziahidi katika iilani ya uchaguzi wa mwaka 2015.
“Halitokuwa jambo jema mimi kutoa milioni 50 kwa kila kijiji nchini wakati huduma mbalimbali kama vile elimu, afya na miundombinu ya barabara na usafirishaji haijakaa vizuri. lakini niwahakikishie kuwa hizo fedha zipo na zitakabidhiwa kwa kila kijiji kama nilivyosema,” alisema Rais Magufuli.
“Inabidi muwe watulivu wakati serikali ikishughulikia matatizo na changamoto zinazohitaji utatuzi wa haraka kabla hatujazitoa fedha hizo,” aliongeza Rais Magufuli.
Rais Magufuli alimtaka pia Mkuu wa mkoa wa mwanza kuhakikisha kuwa anachochea maendeleo ya viwanda na kupitia hivyo nchi itapata maendeleo.

Kiongozi wa Catalonia aliyefutwa "aenda Ubelgiji"

Rais wa Catalonia aliyefutwa Carles Puigdemont ameenda nchini Ubelgiji, wakili wake aliye chini humo anasema.
Wakili huyo Paul Bekaert, hakuzungumzia ripoti kuwa Bw. Puigdemont anajiandaa kuomba kupewa hifadhi.
Mwendesha mashtaka nchini Uhispania ametaka mashataka ya uasi kufunguliwa dhidi yake na viongozi wengine ya kura ya maoni iliyopogwa marufuku.
Serikali ya Uhispania ilichukua udhibiti kamili wa Catalonia siku ya Jumatatu, kuchukua mahala pa viongozi waliofutwa.
Ilifuta utawala wa eneo hilo na kuitisha uchaguguzi mpya baada ya Bw Puigdemont na serikali yake kujitangazia uhuru wiki iliyopita.
Wakili huyo wa Ubelgiji Paul Bekaert alisema kuwa Bw. Puigdemont kwa sasa yuko mji mkuu wa Ubelgiji Brussels.
Mbona Puigdemont akaenda Ubelgiji?
Uhispania ilikuwa imekumbwa na mzozo wa kikatiba tangu kura ya maoni iliyopangwa na serikali ya Bw. Puigdemont, ilipoandaliwa tarehe mosi Oktoba kinyume na amri ya mahakama iliyoamua kuwa kura hiyo ilikuwa kinyume na katiba.
Serikali ya Ctalonia ilisema kuwa asilimia 43 ya wapiga kura walishiriki huku asilimia 90 ya wapiga kura hao wakiunga mkono uhuru

Polisi wawili wasimamishwa kazi

Polisi wawili wa trafiki nchini Afrika Kusini wamesimamishwa kazi na wanakabiliwa na mashtaka ya kuaibisha kikosi cha polisi baada ya video yao "wakila pesa" kusambaa sana mitandao ya kijamii.
Video hiyo inawaonesha polisi hao wawili wakitumia noti za pesa kuchonokoa meno yao na pia kujipangusa, huku muziki wa sauti ya juu ukisikika kwenye gari lao.
Wawili hao wanaonekana pia wakila chakula chao cha mchana kutoka kwenye mikebe ya Styrofoam kwenye sehemu ya kubebea mizigo nyuma ya gari.
Idara ya polisi wa jiji la Ekurhuleni amesema wafanyakazi hao, ambao wamevalia sare rasmi ya polisi wakati huo, wameiaibisha idara hiyo na kwamba vitendo hivyo si vya kistaarabu.
Msemaji wa idara hiyo Wilfred Kgasago amesema wawili hao wamekabidhiwa barua za kuwasimamisha kazi mapema na kwamba watafika katika kamati ya nidhamu Jumanne.

Ndugai:Sina taarifa ya kujiuzulu kwa Nyalandu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai, amesema kwamba hana taarifa za kujiuzulu kwa mbunge wa Singida Kaskazini Lazaro Nyalandu , na wala hiyo barua bado haijamfikia, na kuita kitendo alichokifanya ni umbea.
Job Ndugai ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na mwandishi wa East Africa Radio kwenye kipindi cha East Africa Breakfast, na kusema kwamba Lazaro hakupaswa kutangaza hivyo kabla ya kuhakikisha barua imemfikia.
Pamoja na hayo Spika Ndugai amewataka wabunge wengine kuacha kuwashwa washwa na kufanya mambo ambayo ameyaita ni ya umbea.

Monday, 30 October 2017

MAGAZETI YA LEO JUMANNE YALIVYOPAMBAMWA NA HABARI KATIKA KURASA ZA KWANZA OCT 31 2017


Zitto aingia mikononi mwa Polisi Jumanne ya leo

 Image result for zitto kabwe
taarifa iliyotolewa asubuhi hii na Afisa Habari wa Chama hicho Bwana Abdallah Khamis imeeleza kuwa KIONGOZI wa Chama cha ACT Wazalendo,Zitto Kabwe,amekamatwa na jeshi la Polisi muda huu akiwa nyumbani kwake na anapelekwa kituo cha Polisi Chang'ombe
Sababu za kukamatwa kwake ni hotuba ya juzi Oktoba 29, 2017 katika kata ya Kijichi, Mbagala Jijini Dar es salaam katika uzibduzi wa kampeni za uchaguzi wa mdogo wa madiwani kwenye kata 43 nchini

kituo cha umeme Kipawa chapata hitilafu Gongo la Mboto, Air Port, Chang'ombe wakosa Umeme



Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema hitilafu imetokea katika kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha Kipawa jijini Dar es Salaam.
Taarifa ya Tanesco iliyotolewa leo Jumatatu Oktoba 30,2017 na ofisi ya uhusiano makao makuu imesema hitilafu imetokea saa 11:51 asubuhi.
Kutokana na hitilafu hiyo, Tanesco imesema Gongo la Mboto, Air Port, Chang'ombe na baadhi ya maeneo ya Tabata na Buguruni hayana umeme.
Shirika hilo limesema mafundi wanaendelea na jitihada za kurekebisha hitilafu hiyo na kwa haraka.

Zidane azidi kuumiza kicha na Barcelona

Kocha wa Real Madrid Mfaransa Zinedine Zidane amesema bado timu yake ina muda wa kutosha kuweza kupunguza pointi nane ambazo inazidiwa na vinara Barcelona katika LaLiga msimu huu.
Zidane amesema hayo baada ya timu yake kupoteza mchezo wa jana dhidi ya Girona na kufanya tofauti ya alama kati ya wapinzani hao kuwa nane, Real Madrid ikiwa na alama 20 katika nafasi ya tatu na Barcelona alama 28 kileleni.
Licha ya kupoteza mchezo wa pili msimu huu lakini Zinedine Zidane amesisitiza kuwa mabingwa hao watetezi bado wanaweza kutetea ubingwa wao wa La Liga.
"Najua tunaweza kurejea kwenye ushindi na tukapata pointi na wengine wakapoteza na tukaongoza ligi kwasababu bado muda ni mwingi na mechi bado ni nyingi mpaka msimu ufike mwisho”, amesema Zidane.

IEBC kumtangaza Rais wa Kenya

  Kenya. Tume ya Taifa ya Uchaguzi inatarajiwa kutangaza matokeo ya uchaguzi wa marudio kwa kura ya utais uliofanyika Oktoba 26 na kutangaza ikiwa itaandaa uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa.
Makamu wa Rais wa tume hiyo, IEBC, Consolata Nkatha alisema jana jioni kwamba walikuwa wamepokea matokeo kutoka majimbo sita kati ya saba yaliyokuwa yamesalia na kwamba kufikia Jumatatu asubuhi matokeo yote yatakuwa yamejumlishwa.
“Tumepokea matokeo kutoka majimbo sita sasa na tutakuwa katika nafasi ya kutangaza matokeo ya mwisho kesho (leo) asubuhi. Tutafanya kazi usiku kucha kuhakikisha uhakiki na ujumlishaji unakamilika. Pia tutatangaza ikiwa tutaendesha uchaguzi katika majimbo 25 ambako uliahirishwa au la,” alisema Nkatha.
Majimbo hayo yaki kwenye kaunti ambazo tume iliahirisha uchaguzi ambazo ni Kisumu, Migori, Siaya na Homa Bay.
Mawasiliano na IEBC yamekuwa haba lakini inafahamika kwamba makamishna wa tume walifanya kikao cha saa kadhaa na wanasheria wao juzi kufikiria kama wajaribu kuitisha uchaguzi katika majimbo 25.
Jana jioni Mwenyekiti wa IEBC, Wafula Chebukati alisema tume yake ilikuwa imehakiki matokeo ya majimbo 259 kati ya 265, yakiwemo ya nchi za nje.
Kutoka katika majimbo hayo, Chebukati alisema watu 7,447,014 walijitokeza kupiga kura sawa na asilimia 43.04. Matokeo yaliyokuwa yakitangazwa moja kwa moja kutoka jengo la Bomas of Kenya Rais Kenyatta alijikusanyia kura 7,393,405 sawa na asilimia 98.3 ya kura halali.

Nyalandu atimkia Chadema

NIMEAMUA kujiuzulu NAFASI yangu ya Ujumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi CCM, pamoja na nafasi zote za Uongozi ndani ya Chama kuanzia leo, Oktoba 30, 2017.
 HALIKADHALIKA, asubuhi ya leo nimemwandikia Spika wa Bunge, Mh. Job Ndugai, Mb., barua ya kujiuzulu nafasi yangu ya UBUNGE wa Jimbo la Singida Kaskazini kupitia tiketi ya CCM, nafasi ambayo nimeitumikia kwa vipindi vinne mfululizo tangu nilipochaguliwa kwa mara ya kwanza mnamo mwaka 2000 hadi Sasa.
AIDHA, Nimechukua UAMZI huo kutokana na kutorishwa kwangu na mwenendo wa hali ya Kisiasa nchini, ikiwa ni pamoja na ukiukwaji wa HAKI za Kibinadamu, ongezeko la vitendo vya dhuluma wanavyofanyiwa baadhi ya watanzania wenzetu, na kutokuwepo kwa mipaka ya wazi kati ya MIHIMILI ya dola (Serikali, Bunge, na Mahakama) kunakofanya utendaji kazi wa Kibunge wa Kutunga Sheria na wa Kuisimamia Serikali kutokuwa na uhuru uliainishwa na kuwekwa bayana KIKATIBA.
VILEVILE, Naamini kwamba bila Tanzania kupata Katiba Mpya Sasa, hakuna namna yeyote ya kuifanya mihimili ya dola isiingiliane na kuwepo kwa ukomo wa wazi na kujitegemea kwa dhahiri kwa mihimili ya Serikali, Bunge na mahakama ambayo ndio chimbuko la Uongozi Bora wa nchi, na kuonesha kwa uwazi kuwa madaraka yote yatokana na wananchi wenyewe, na kwamba Serikali ni ya Watu kwajili ya Watu.
MIMI Naondoka na kukiacha Chama Cha Mapinduzi CCM, nikiwa nimekitumikia kuanzia ngazi ya Uenyekiti wa UVCCM Mkoa, Ujumbe wa Kamati za Siasa Wilaya na Mkoa, Ujumbe wa Kamati ya Wabunge Wote wa CCM na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM TAIFA,  kwani nimejiridhisha kuwa kwa mwenendo wa hali ya kisiasa, kiuongozi na kiuchumi uliyopo Tanzania Sasa, CCM imepoteza mwelekeo wake wa kuisimamia Serikali kama ilivyokuwa hapo awali. AIDHA, Naamini kuwa, kama ilivyotokea kwa mihimili ya Bunge na Mahakama kutokuwa na uhuru kamili, bila kuingiliwa kiutendaji kwa namna Moja au nyigine, CCM nayo imekuwa Chini ya miguu ya dola badala ya chama kushika hatamu na kuikosoa Serikali inapobidi kama yalivyokuwa maono ya Baba wa TAIFA MWALIMU Julius Kambarage Nyerere.

HIVYOBASI, kwa dhamira yangu, na kwa uamuzi wangu mwenyewe, nikiwa na haki ya KIKATIBA, natangaza KUKIHAMA Chama Cha Mapinduzi CCM leo hii, na nitaomba IKIWAPENDEZA wanachama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, basi waniruhusu kuingia MALANGONI mwao, niwe mwanachama, ili kuungana na CHADEMA na watanzania wote wanaopenda kuleta mabadiliko ya kisiasa na kiuchumi nchini kwa kupitia mfumo wa ki demokrasia na uhuru wa mawazo.

Saturday, 28 October 2017

ZILIZOONEKANA KATIKA KURASA ZA MBELE KUPITIA MAGAZETI YA LEO JUMAPILI OCT 29 2017




Udart yapata hasara

 Image result for mvua dar kuharibu miundo mbinu ya mabasi mwendokasi
Mvua kubwa iliyonyesha jijini Dar es Salaam kwa siku mbili imesababisha kampuni ya Usafiri wa Mabasi Yaendayo Haraka (Udart) kuhamisha baadhi ya shughuli eneo la Jangwani.
Mbali ya kuathiri shughuli katika eneo hilo, Udart imesema mvua iliyonyesha Jumatano Oktoba 25 na Alhamisi Oktoba 26,2017 imesababisha mabasi 29 ya kampuni hiyo kuharibika.
Udart imehamisha huduma za kulaza magari, ujazaji wa mafuta na gereji.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano cha Udart, Deus  Bugaywa amesema leo Jumamosi Oktoba 28,2017 kuwa vituo vya Gerezani na Kimara ndivyo vitatoa huduma ya gereji.
Amesema vituo vya Kivukoni, Gerezani na Kimara vitatoa huduma ya kulaza magari na kuyajaza mafuta.
Bugaywa amesema mvua imeathiri mabasi 29 kati ya 134 yanayotoa huduma jijini Dar es Salaam.
Amesema vifaa vya mabasi vimesombwa na maji na pia baadhi ya vyumba vya ofisi vimeharibiwa.
"Kwanza, tunawaomba msamaha wateja kwa usumbufu uliojitokeza Alhamisi wakati wa mvua. Kwa sasa watuvumilie hadi Jumapili Oktoba 28,2017 huduma zitakaporejea vizuri. Mabasi 29 yalishindwa kuendelea na huduma baada ya kuathiriwa na mvua," amesema Bugaywa akizungumza na waandishi wa habari.
Amesema, "Mabasi hayo yalikuwa kwenye marekebisho katika injini, giaboksi na difu. Mvua zilipoanza maji yalijaa na matengenezo yalisimama. Kwa sasa mafundi wanaangalia athari na namna gani zishughulikiwe mapema ili magari yarudi barabarani."
Bugaywa amesema kwa sasa si rahisi kuwa na makadirio ya hasara iliyotokana na mvua.
Alipoulizwa kuhusu hatima ya kutumia majengo ya ofisi yaliyopo Jangwani, Bugaywa amesema suala hilo linahitaji majadiliano kati ya Serikali na wadau wote wanaohusika katika mradi huo.

Polisi wawili wauawa kwa kupigwa risasi

Polisi wawili waliokuwa kituo cha Polisi Kayole Nairobi wameuawa kwa kupigwa risasi na kisha wauaji kuondoka na bastola walizokuwa nazo
Maafisa polisi wenzake kutoka kambi ya polisi ya Kirima waliikuta miili yao barabarani asubuhi ya leo
Mafisa hao wametambuliwa kuwa ni Konstebo Linus Inima and James Gitahi.
Maafisa wa polisi wamekuwa wakipambana na waandamanaji wanaopinga uchaguzi na eneo la Kayole huko Nairobi ni kati ya maeneo yaliyoathiriwa na vurugu hizo, ila haijajulikana kama mauaji ya polisi hao yanahusiana na uchaguzi

Kampuni zashindania kukuza bangi Denmark

Image result for bangi
Kampuni nchini Denmark zimeanza kuwasilisha maombi kwa serikali kupata idhini ya kukuza bangi kujiandaa kwa wakati ambao bangi itakuwa halali nchini humo mwaka ujao.
Kampuni 13 tayari zimewasilisha maombi kwa idara ya serikali inayohusika ya Laegemiddelstyrelsen.
Bangi itakuwa halali kutumiwa kama dawa na watu wanaotatizwa na magonjwa yenye uchungu mwingi kama vile saratani na kuganda kwa misuli.
Kuanzia Januari 2018, bangi itakuwa inatolewa kama dawa kwa wagonjwa kwa majaribio ya kipindi cha miaka minne.
Gazeti la Copenhagen Post linasema kuanzia wakati huo, wagonjwa wanaweza kupendekezewa bangi kama dawa na daktari nchini humo.
Lakini bunge bado linajadiliana kuhusu mfumo utakaotumiwa.
Hilo limezifanya kampuni kubwa za kilimo cha mboga na matunda nchini humo kama vile Dansk Gartneri ya Jorgen K. Andersen kutowasilisha maombi kwa sasa.
Bw Andersen ameambia tovuti ya fyens.dk kwamba kampuni yake inatazamia kwamba kutakuwa na mkanganyiko mkubwa katika kutolewa kwa idhini ya kukuza bangi.
Baadhi ya kampuni hata hivyo zinakusudia kukuza sekta ya bangi Denmark na kuuza dawa hiyo maeneo mengine ya nje ambapo bangi ni halali.

Kichuya awaondoa hofu mashabiki wa Simba

Kiungo mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya amewaondoa hofu mashabiki wa timu hiyo kuelekea mchezo wao wa leo dhidi ya Yanga, kwamba wapinzani wao hao ni wepesi na watawafunga leo.
Kichuya amewataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi uwanjani bila ya hofu kwani ana uhakika wa ushindi kutokana na maandalizi yao chini ya Kocha Joseph Omog.
Kichuya alisema, katika mechi hiyo kikubwa wao kama wachezaji wamepania kupata ushindi ili waendelee kubaki kileleni katika msimamo ya ligi.
 “Tunajua kabisa mashabiki wa Simba kitu gani wanakitaka katika mechi hii dhidi ya Yanga, hivyo niwatoe hofu kwa kuwaambia kuwa waje kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kutushangilia.
“Watarajie matokeo mazuri ya ushindi na soka safi kutoka kwetu kutokana na maandalizi tuliyoyafanya kambini Zanzibar, sisi wachezaji tunataka pointi tatu ili tubaki kileleni,” alisema Kichuya.

Kikosi cha Yanga kitakachovaana na Yanga

KIKOSI CHA YANGA:

1. Youthe Rostand

2. Juma Abdul

3. Gadiel Michael

4. Andrew Vicent

5. Kelvin Yondani

6. Papy Tshitshimbi

7. Pius Buswita

8. Raphael Daud

9. Obrey Chirwa

10. Ibrahim Ajibu

11. Geofrey Mwashiuya

Kikosi cha Simba kitakachomenyana na Yanga


KIKOSI CHA SIMBA:

1. Aishi Manula

2. Erasto Nyoni

3. Mohamed Zimbwe (C)

4. Juuko Murshid

5. Method Mwanjale

6. Jonas Mkude

7. Shiza Kichuya

8. Muzamiru Yassin

9. John Bocco

10. Emmanuel Okwi

11. Haruna Niyonzima

Friday, 27 October 2017

MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI OCT 28 2017




Watu wanne wafariki kutokana na mvua ya jana

 Image result for lazaro mambosasa
  Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema watu wanne wamekufa kufuatia mvua iliyonyesha jana Alhamisi.
"Jana tulipokea taarifa za watu wawili leo Ijumaa asubuhi tumepokea taarifa za watu wawili tena hivyo mpaka sasa tuna idadi ya watu wanne," amesema.
Amesema bado wa naendelea kukusanya taarifa.

Homa ya Simba na Yanga yazidi kupanda kwa kasi kubwa

Kikosi cha Simba kinatarajia kurejea jijini Dar es Salaam leo kwa maandalizi ya mwisho ya mechi yao ya kesho dhidi ya Yanga.
Simba walikuwa kambini mjini Zanzibar kujiandaa na mechi ya Ligi Kuu Bara itakayopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Taarifa zinaeleza, Simba watawasili kwa kutumia ndege za kukodi tayari kwa ajili ya mechi hiyo.
Kikosi hicho kitaingia kambini jijini Dar es Salaam kwa ajili ya maandalizi ya mwisho.
Hata hivyo, Simba wamekuwa wakifanya uficho kuhusiana na sehemu watakayokaa jijini Dar es Salaam wakimalizia maandalizi yao hayo ya mwisho kabla ya kesho.

Burundi yajiondoa rasmi katika mahakama ya ICC

Rais Nkurunziza alichukua madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.
Burundi limekuwa taifa la kwanza mwanachama wa mahakama ya kimataifa kuhusu uhalifu wa jinai kujiondoa katika mahakama hiyo.
Serikali ya taifa hilo la Afrika ya kati liliuarifu Umoja wa Mataifa UN kuhusu hatua hiyo mwaka mmmoja uliopita , na hii leo kujitoa kwao kunaanza kuidhinishwa rasmi.
Inaonekana kama kipimo cha jamii ya kimataifa kuhusu haki.

Ni hatua sio ya kawaida.
Je kutakuwa na athari zake na ni kwa nini ni muhimu?.
Kulingana na mwandishi wa BBC Anna Holligan kujiondoa kwa Burundi ni majuto makubwa.
Mahakama ya ICC imeanza kutathmini iwapo inaweza kuchunguza ghasia za kisiasa zilizoibuka baada ya rais Nkurunziza kuchukuwa madaraka kwa awamu ya tatu, licha ya kuwepo kwa kipindi cha mihula miwili katika katiba ya taifa hilo.
ICC bado ina uwezo kuchunguza uhalifu uliotekelezwa wakati Burundi ilipokuwa mwanachama wa mahakama hiyo.
Lakini haiwezi kuchunguza uhalifu wowote wa siku zijazo.

Wakenya 6,553,858 wamepiga kura

Mwenyekiti wa IEBC Wafula Chebukati amedai kwenye ukurasa wake wa Twitter kwamba Wakenya wapatao 6,553,858 wamejitokeza na kupiga kura. Hii idadi imejumuishwa kutoka kwa maeneo bunge 267 nchini.
Awali alitangaza kuahirisha uchaguzi kwenye gatuzi nne za mkoa wa Nyanza baada ya wafuasi wa Raila wamekinukisha kule na kuvuruga shughuli za upigaji wa kura kufanyika. Hivyo ameahirisha hadi Jumamosi.

Meli ya uvuvi ya K Kusini yaachiwa huru Korea Kaskazini

Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria, chombo cha habari kimesema.
Meli hiyo na wafanyikazi wake itaachiliwa katika mpaka wa kijeshi katika bahari ya mashariki kulingana na chombo cha habari cha KCNA.
Uamuzi huo ulitolewa baada ya wafanyikazi hao kuomba msamaha kwa kufanya makosa hayo, kiliongezea.
Hatua hiyo inajiri wakati ambapo kuna wasiwasi katika eneo hilo huku pande zote mbili zikifanya mizururu ya mazoiezi ya kijeshi.
Korea Kaskazini imesema kuachiliwa kwa meli hiyo ya uvuvi, baadaye siku ya Ijumaa inafuatia hatua ya kukiri makosa kwa wale waliokuwa wakiabiri chombo hicho ambao walitaka serikali ya Korea Kaskazini kuwavumilia.
Uchunguzi, kulingana na Korea Kaskazini, ulithibitisha kuwa wavuvi hao waliingia maji ya taifa lake siku ya Jumamosi.

Thursday, 26 October 2017

ZILIZOSHIKA HATAMU KATIKA MAGAZETI YA LEO IJUMAA OCT 27 2017




Kukosekana kwa Umeme kwa muweka pabaya Meneja uendeshaji wa kituo cha umeme Kidatu


Waziri wa Nishati, Medard Kalemani amemtaka Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Abdallah Ikwasa kumuondoa mara moja meneja uendeshaji wa kituo cha umeme  Kidatu akituhumiwa kwa uzembe.
Dk Kalemani amesema hayo leo Alhamisi Oktoba 26,2017 baada ya kukosekana umeme nchi nzima jana Jumatano Oktoba 25,2017 kwa takriban saa 10, huku kukiwa hakuna ufafanuzi wa kueleweka.
Waziri amemtaka meneja huyo kuandika barua ya kujieleza ndani ya saa tatu ni kwa nini asiondolewe katika nafasi hiyo.
Dk Kalemani pia amempa siku tatu Meneja Udhibiti wa Mitambo, Mhandisi Izihaki Mosha kujieleza ni kwa nini anastahili kubaki katika nafasi hiyo.
Mbali na maagizo hayo, waziri amemtaka Ikwasa; Naibu Mkurugenzi Usafirishaji, Mhandisi Bishaija Kahitwa na Mosha kuandika barua za kuachia nafasi zao iwapo umeme hautarudi siku nzima leo.
“Siwaondoi, bali nataka umeme usiporudi muondoke wenyewe katika nafsi zenu kwa sababu hii kazi itakuwa imewashinda,” amesema.
Dk Kalemani amesema, “Haiwezekani umeme ukatike nchi nzima ndani ya saa 10 na bado hamjajua tatizo ni nini, wananchi wanatuma ujumbe mfupi kila kona wameunguliwa vitu vyao, wameunguliwa mashine zao nani atalipa hizo gharama.”
Waziri aliyefanya ziara kwenye mitambo ya kuzalisha umeme Ubungo na Kinyerezi I jijini Dar es Salaam kubaini chanzo cha kukatika kwa umeme nchi nzima, amesema wakati wa kufanya kazi kwa mazoea umekwisha.

Thailand kuuchoma mwili wa hayati mfalme Bhumibol Adulyadej

Waombolezaji kote Thailand wanafanya matembezi kunaadhimisha sehemu kuu ya siku tano za sherehe za mazishi kwa ajili the Mfalme Bhumibol Adulyadej aliyeaga dunia.
Mfalme huyo alifariki Oktoba 2016 akiwa na umri wa miaka 88, Mwili wake utateketezwa kwa moto baadaye Alhamisi, Kwa taratibu za kifalme zitakazoongozwa na mwanae na mrithi wake, Mfalme Maha Vajiralongkorn.
Taratibu za mazishi zilianza Jumatano kwa sherehe za kubudha ,kwenye kasri Kuu la kifalme, Leo Alhamisi imetangazwa kuwa siku ya mapumziko, ambapo biashara nyingi zitafungwa kwa siku ama kwa nusu siku.
Mapema Alhamisi, mwili wa mfalme huyo utaletwa kwenye eneo maalum utakapochomwa kutoka kwenye Ukumbi waKifalme ulipo katika Kasri kuu kwa ajili ya uteketezwa.
Wajumbe wa familia ya ufalme wa Thailand na waheshimiwa kutoka nchi 40 watahudhuria mazishi hayo ya kuchomwa kwa mwili wa hayati mfalme Bhumibol Adulyadej , huku umati mkubwa wa watu ukitarajiwa kujipanga kwenye mitaa ya karibu.

Mafuriko Dar hatari kubwa

Mvua ya inayoendelea kunyesha kwa siku mbili mfululizo katika jiji la Dar es salaam, imesababisha mafuriko makubwa katika maeneo mbalimbali Jijini humo, ikiwemo eneo la Jangwani ambapo maji hayo yamefunga mawasiliano ya barabara ya Morogoro, Hakuna gari inayokwenda wala kurudi mjini.
Mpaka sasa umeripotiwa kuokotwa katika mto kenge uliopo Tabata jijini humo, mwili wa mtu mmoja mwenye jinsia ya kiume.
Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka.
Wakaazi wa eneo la Jangwani wakiwa wanaendelea kuopoa baadhi ya mali zao
Abiria wakiwemo Wanafunzi wakiwa wamekwama katika kituo cha mabasi yaendayo haraka cha Jangwani, Dsm.


Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amefika katika eneo hilo nakuwataka wananchi kuondoka katika maeneo hayo kwasasa kwakuwa maji yanaendelea kuongezeka.

Mbunge wa Ilala Musa Zungu amefika na kueleza kuwa mafuriko hayo ni makubwa ingawa mpaka sasa hawajapata takwimu sahihi ya uharibifu unaotokana na mafuriko hayo.