WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
ametembelea kiwanda cha kampuni ya SBC Tanzania Ltd kinachotengeneza
vinywaji baridi pamoja na kiwanda cha kiwanda cha kukata na kung’arisha
mawe ya asili (mabo) cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, vilivyoko
katika eneo la Iyunga Mjini Mbeya.
Amevitembelea viwanda hivyo kwa
lengo la kukagua utekelezaji wa sera ya kujenga uchumi wa viwanda
nchini, ambao ndiyo kipaumbe cha Serikali ya Awamu ya Tano. Waziri Mkuu
alivitembelea viwanda hivyo jana jioni (Jumatatu, Julai 31, 2017), akiwa
katika ziara yake ya kikazi mkoani Mbeya.
Akiwa katika kiwanda cha Pepsi,
Waziri Mkuu alikagua maendeleo ya ujenzi wa upanuzi wa kiwanda hicho
kwa ajili ya kuanza uzalishaji wa vinywanji baridi kwenye chupa za
plastiki, ambapo amewasihi Watanzania kupenda kutumia bidhaa
zinazozalishwa kwenye viwanda vya ndani.
Pia Waziri Mkuu aliishauri
kampuni hiyo kuendelea kupanua uwekezaji wake hapa nchini kwa kuwa
Tanzania ina sera na mazingira mazuri ya uwekezaji. Kiwanda hicho
kilijengwa mwaka 1999 kikiwa na wafanyakazi 75 na kwa sasa kina
wafanyakazi 190.
“Nawashauri muendelee kuwekeza Tanzania kwani mbali na utulivu wa kisiasa pia sera na mazingira yake ya uwekezaji ni mazuri.”
Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi
kampuni SBC Tanzania Ltd. Bw. Atif Dar alisema kiwanda cha Mbeya ni cha
pili kwa ukubwa wa mauzo ya vinywaji baridi vinavyotengenezwa na kampuni
hiyo kikitanguliwa na kiwanda cha mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema kwa sasa wanachukua soda
zilizofungwa katika chupa za plastiki kutoka katika kiwanda chao cha Dar
es Salaam, ambapo waliamua kupanua kiwanda hicho ili waanze kutengeneza
soda zilizofungwa katika chupa za plastiki mkoani Mbeya baada ya
mahitaji kuongezeka.
Bw. Dar alisema gharama za
uwekezaji huo ni dola za Marekani milioni 3.5, ambapo mradi huo
unatarajiwa kuanza rasmi Novemba 2017 ambapo mbali na kuuza katika soko
la mikoa ya Nyanda za Juu Kusini pia watasafirisha katika nchi za Zambia
na Malawi.
Pia Bw. Dar alimkabidhi Waziri
Mkuu hundi ya sh. milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vifaa tiba
katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mbeya, ikiwa ni sehemu ya mchangamo
wa kiwanda hicho katika uboreshaji wa shughuli mbalimbali za kijamii.
Awali Waziri Mkuu alitembelea kiwanda cha Marmo Granito Mines Tanzania Ltd
Waziri Mkuu alisema mbali na
kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo
vitakavyowawezesha wananchi tununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na
ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.
Pia aliwataka Watanzania wote
hususani mashirika, taasisi, asasi na mamlaka za Serikali kujenga
utamaduni wa kupenda kununua na kutumia na bidhaa mbalimbali
zinazozalishwa na viwanda vilivyopo hapa nchini ili viweze kuimarika na
kusaidia kutatua tatizo la ajira.
Alitoa kauli hiyo badaa ya
kutembelea kiwanda cha kukata na kung’arisha mawe ya asili (mabo) cha
Marmo Granito Mines Tanzania Ltd, kilichoko katika eneo la Iyunga Mjini
Mbeya. Kiwanda hicho kinatumia malighafi za hapa nchini.
Waziri Mkuu alisema mbali na
kukuza uchumi na kuongeza fursa za ajira nchini, viwanda hivvyo ndivyo
vitakavyowawezesha wananchi kununua bidhaa kwa bei nafuu tofauti na
ilivyo sasa kwa kuwa vitu vingi vinaagizwa kutoka nje ya nchi.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMANNE, AGOSTI 1, 2017
No comments:
Post a Comment