Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni
ya usajili wa Gazeti la Daily News mwakilishi wa gazeti hilo Bi.
Pudenciana Temba. Idara ya Habari imetoa imetoa leseni nne kwa ambapo
leseni namba moja imetolewa kwa Jarida la Nchi Yetu linalotolewa na
Idara hiyo, namba mbili imetolewa kwa HabariLeo, namba tatu Dailynews na
nne imetolewa kwa Spotileo.Katikati ni Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya
Habari (MAELEZO) Usajili Bw. Patrick Kipangula.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimkabidhi leseni
ya usajili wa Gazeti la HabariLeo mwakilishi wa gazeti hilo mhariri wa
gazeti hilo Bw. Amir Mhando leo Jijini Dar es Salaam. Leseni hiyo
imetolewa kufuatia kuanza kwa matumizi ya sheria mpya ya Huduma za
Habari ya mwaka 2016.
Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya
Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti ya Daily News, HabariLeo
na SpotiLeo Dkt. Jim Yonaz akisisitiza jambo mara baada ya kumalizika
kwa zoezi la kutolewa kwa Leseni za magazeti ya Kampuni yake kumalizika
leo Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akimpongeza Mhariri
Mtendaji wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) inayomiliki magazeti
ya Daily News, HabariLeo na SpotiLeo, Dkt. Jim Yonaz kwa Kampuni yake
kuzingatia matakwa ya Sheria ya Huduma za Habari ya mwaka 2016 kwa
kujisajili upya na kupatiwa leseni.
Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari
(MAELEZO) na Msemaji wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi akiwa katika picha
ya pamoja na wahariri wa magazeti ya HabariLeo, DailyNews, SpotiLeo
yanayomilikiwa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) pamoja na
uongozi wa Idara ya Habari (MAELEZO) mara baada ya kukabidhiwa Lesini za
usajili wa magzeti hayo leo Jijini Dar es Salaam.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO
Na. Neema Mathias na Paschal Dotto- MAELEZO.
Serikali kupitia Idara ya Habari
(MAELEZO) imeanza rasmi utekelezaji wa Sheria ya Huduma za Habari kwa
kutoa leseni kwa vyombo vya machapisho yakiwemo Magazeti na Majarida.
Akizungumza katika makabidhiano ya
leseni hizo Jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Idara ya Habari
MAELEZO na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema utoaji
wa leseni ni utekelezaji wa agizo rasmi lililotolewa Agosti 23, 2017
lililowataka wamiliki wote wa machapisho kujisajili upya na kupewa
leseni kwa lengo la kuifanya tasnia ya Habari kuwa taaluma rasmi kama
zingine.
“Leseni hizo zimeanza kutolewa
rasmi Agosti 23 na zoezi hilo litaendelea hadi Oktoba 15, 2017 na baada
ya hapo wale amabo watachapisha magazeti na majarida bila kuzingatia
Sheria hiyo watakuwa wametenda kosa la jinai”, alisema Dkt. Abasi.
Katika zoezi hilo Dkt. Abbasi
alitoa leseni kwa vyombo vinne ambavyo ni Jarida la Nchi Yetu
linalomilikiwa na Idara ya Habari MAELEZO, gazeti la Daily News, Habari
Leo pamoja na Spoti Leo ambayo ni magazeti ya Serikali.
Dkt. Abbasi ametoa wito kwa vyombo
vingine vya habari ambavyo bado havijaanza taratibu za upataji wa
leseni visisubiri hadi dakika za mwisho za mchakato huo ili kuepuka
msongamano na usumbufu usio wa lazima.
“Nitumie fursa hii kuwaalika ambao
hawajapata leseni wafanye haraka, Tanzania Standard Newspaper (TSN)
walitimiza masharti ndani ya siku tatu ndio maana leo wamepata leseni
hizo, hakuna urasimu wala nia mbaya ya kufungia baadhi ya machapisho
kama wengi wanavyodai bali ni katika kutekeleza matakwa ya Sheria”,
alisisitiza Dkt. Abbasi.
Kwa upande wake Mhariri Mtendaji
wa TSN Dkt. Jim Yonazi ameviasa Vyombo vingine vya Habari kutekeleza
agizo hilo ili kupata uhuru mpana katika uwajibikaji pamoja na kuwa
mfano wa kutii Sheria bila shuruti ili taaluma ya habari iendelee
kuheshimika kwa jamii.
“Ukifanya kazi kihalali unakuwa na
uhuru wa kufanya kazi vizuri, ubunifu unaongezeka na unafanya biashara
bila wasiwasi”, alisisitiza Dkt.Yonazi.
No comments:
Post a Comment