Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa
Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake
mjini Maputo,Msumbiji mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake
Ikulu jijini Dar Es Salaam
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiagana na Balozi wa
Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun mwenye makazi yake
mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari
ambao wameonyesha utayari wa kuwekeza nchini Tanzania.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya
pamoja na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre Jhumun
mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji , Wawekezaji wa Uzalishaji
Sukari na Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio .
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya
mazungumzo na Balozi wa Mauritius nchini Tanzania Mhe. Jean Pierre
Jhumun mwenye makazi yake mjini Maputo,Msumbiji aliyeongozana na
Wawekezaji wa Uzalishaji Sukari ambao wameonyesha nia na utayari wa
kuwekeza nchini.
Mbali ya ujumbe kutoka Mauritius, wengine waliohudhuria mazungumzo hayo ni Mkurugenzi Mkuu wa NSSF Profesa Godius Kahyarara na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, Bw.William Erio .
Katika mazungumzo hayo Makamu wa
Rais amewahakikishia wawekezaji hao ushirikiano wa Serikali na kuwaeleza
kuwa Tanzania ina mazingira bora ya uwekezaji.
Mbali ya fursa ya uwekezaji katika Sukari, Makamu wa Rais aliainisha maeneo mengine ya kuwekeza kama vile viwanda na TEHAMA.
Aidha alisema pindi uwekezaji huo
ukifanikiwa , Tanzania itafaidika na soko la nchi za Jumuiya ya Afrika
Mashariki (EAC) na Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) na
masoko mengine duniani kwa ujumla.
Uwekezaji huu utakuwa wa Ubia kati mashirika ya hifadhi ya mifuko ya jamii na pia kampuni nyingine za wazawa.
No comments:
Post a Comment