Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania, Wallace Karia amewateua Makamu wa Rais wa zamani wa TFF,
Athuman Nyamlani na Ahmed Mgoyi kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya
TFF.
Rais Karia ameteua kwa kwa mujibu
wa mamlaka aliyonayo katika Katiba ya TFF ikiwa ni wiki moja baada ya
kupatikana kwa viongozi wa shirikisho katika uchaguzi mkuu uliofanyika
Agosti 12, mwaka huu.
Rais Karia aliwatambulisha
viongozi hao kwenye Kikao cha Kamati ya Utendaji iliyofanyika Jumanne
Agosti 22, mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Katika kikao hicho pia Rais Karia
alitumia fursa hiyo kutangaza viongozi wa kamati mbalimbali za TFF
zikiwamo za kinidhamu na kisheria.
Kamati ya Nidhamu: Mwenyekiti
Tarimba Abbas, Makamu Mwenyekiti, Peter Hella wakati wajumbe ni Boniface
Lyamwike, Dk. Bill Haonga na Kassim Dau.
Kamati ya Rufani za Nidhamu:
Mwenyekiti ni Wakili Rahim Zuber Shaban; Makamu Mwenyekiti, Stella
Mwakingwe wakati Wajumbe ni Abbas Mtemvu, Amani Mulika na Siza Chenja.
Kamati ya Maadili: Mwenyekiti ni
Wakili Hamidu Mbwezeleni, Makamu Mwenyekiti ni Wakili Steven Zangira
wakati Wajumbe ni Glorious Luoga, Walter Lungu na Amin Bakhressa.
Kamati ya Rufaa ya Maadili:
Mwenyekiti ni Wakili Ebenezer Mshana; Makamu Mwenyekiti ni DCP. Mohammed
Mpinga na wajumbe ni Wakili Benjamin Karume, George Mayawa na ASP.
Benedict Nyagabona.
Kamati ya Uchaguzi: Mwenyekiti ni
Revocatus Kuuli; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Mohammed Mchengerwa; Wakili
Edwin Mgendera; Wakili Kiomoni Kibamba na Wakili Thadeus Karua.
Kamati ya Rufani ya Uchaguzi:
Mwenyekiti ni Kenneth Mwenda; Makamu Mwenyekiti ni Jabir Shekimweri na
Wajumbe ni Wakili Rashid Sadalla, Irene Kadushi na Mohammed Gombati.
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi
za Wachezaji: Mwenyekiti ni Elias Mwanjala; Makamu Mwenyekiti ni Wakili
Malangwe Mchungahela wakati Wajumbe ni Zakaria Hanspope, Robert
Selasela, Goodluck Moshi, Mhandisi Issa Batenga na Hamis Semka.
Kamati ya Fedha na Mipango:
Mwenyekiti ni Michael Wambura; Makamu Mwenyekiti ni Francis Ndulane na
Wajumbe ni Almas Kasongo, Pascal Kihanga, Maximillian Tabonwa, Paul
Bilabaye na Farid Abeid.
Kamati ya Mashindano: Mwenyekiti
ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni James Mhagama wakati Wajumbe ni
Kenneth Pesambili, Shafii Dauda, Fortunatus Kalewa na Mhandisi Andrew
Makota.
Kamati ya Ufundi: Mwenyekiti ni
Vedastus Lufano; Makamu Mwenyekiti ni Issa Bukuku na wajumbe ni Sarah
Chao, Ally Mayay, Michael Bundala, Omar Abdulkadir na Israel Mujuni.
Kamati ya Soka la Vijana:
Mwenyekiti ni Khalid Abdallah; Makamu Mwenyekiti ni Lameck Nyambaya na
Wajumbe ni Mohammed Aden, Ramadhani Nassib, Salim Kibwana na Vicent
Majili.
Kamati ya Mpira wa Wanawake:
Mwenyekiti ni Amina Karuma; Makamu Mwenyekiti ni Rose Kissiwa na Katibu
wa Kamati hiyo ni Somoe Ng’itu wakati Wajumbe ni Zena Chande, Beatrice
Mgaya, Sofia Tigalyoma, Zuhura Kapama na Nia Mjengwa.
Kamati ya Waamuzi: Mwenyekiti ni
Saloum Chama; Makamu Mwenyekiti Joseph Mapunda wakati Wajumbe ni Nassib
Mabrouk, Leslie Liunda na Soud Abdi.
Kamati ya Habari na Masoko:
Mwenyekiti ni Dunstan Mkundi; Makamu Mwenyekiti ni Mbasha Matutu wakati
Wajumbe ni Imani Kajura, Mgaya Kingoba, Godfrey Dilunga na Samson
Mbamba.
Kamati ya Ukaguzi wa Fedha:
Mwenyekiti ni Yahya Hamad; Makamu Mwenyekiti ni Athuman Nyamlani na
Wajumbe ni Khalifa Mgonja, Japhary Kachenje, Jackson Songoro na Benesta
Rugora.
Kamati ya Tiba: Mwenyekiti ni Dkt.
Paulo Marealle; Makamu Mwenyekiti ni Dkt. Fred Limbanga Wakati wajumbe
ni Dkt. Norman Sabun, Dkt. Lisobina Kisongo, Dkt. Eliezer Ndalama, Dkt.
Elson Maeja na Violet Lupondo.
Kamati ya Futsal na Beach Soccer:
Mwenyekiti ni Ahmed Mgoyi; Makamu Mwenyekiti ni Hussein Mwamba na
Wajumbe ni Blassy Kiondo, Isaac Munisi, Didas Zimbihile na Aaron Nyanda.
Kamati ya Ajira: Mwenyekiti ni
Issa Bukuku; Makamu Mwenyekiti ni Saloum Chama wakati Wajumbe ni Athuman
Kihamia, Mtemi Ramadhani, Noel Kazimoto na Hawa Mniga.
Kamati ya Leseni za Klabu:
Mwenyekiti ni Wakili Lloyd Nchunga; Makamu Mwenyekiti Wakili Emmanuel
Matondo wakati Wajumbe ni Profesa Mshindo Msolla, Hamisi Kissiwa na
David Kivembele.
Kamati ya Rufaa za Leseni:
Mwenyekiti Wakili Dk. Damas Ndumbaro; Makamu Mwenyekiti ni Wakili Alex
Mngongolwa Wajumbe ni Meneja wa zamani wa Uwanja wa Taifa, Charles
Matoke, Tumainiel Mlango na Ahmed Menye.
No comments:
Post a Comment