Tuesday, 1 August 2017

Hali ya kibiti ni shwari

Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini Kamishina Msaidizi wa Polisi (ACP) Barnabas Mwakalukwa.
 unaoendelea kwa sasa.
ACP Mwakalukwa amebainisha hayo wakati alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha East Africa Breafast kinachoongozwa na Shaaban Luppa pamoja na Irene Tillya kutoka East Africa Radio kuhusu uhusiano kati ya polisi na raia ikiwa ni siku chache kupita tokea taasisi ya Twaweza kufanya utafiti wake na kubaini kuwa ni asilimia 74 ya watanzania ambao hawatoi taarifa katika jeshi la polisi wanapopatwa na athari ya uhalifu katika maeneo yao yanayowazunguka.
"Watu wasiwe na hofu ya kuja kuwekeza Tanzania na hata tafiti ziwe zinafanyika kwa ajili ya kuijenga Tanzania yenye amani na utulivu na zitusaidie sisi wasimamizi wa sheria, tusimamie sheria vizuri watu waendelee kwa maana sasa wananchi  wamechoka kusikia maovu yanayofanyika, wanataka kusikia mema yanayofanyika .
Tumeona uhalifu umepungua mpaka tunaongelea suala la watu kujichukulia sheria mkononi hatuongelei upolaji wa kutumia silaha, ujambazi wa mabenki tuliyozoea", amesema ACP Mwakalukwa.
ACP Mwakalukwa ameendelea kwa kusema kuwa "kuna nchi nyingine suala la uhalifu siyo jambo la kuzungumzia huwa wao wanazungumzia maendeleo waliyokuwa nayo. Kwa hiyo tangazeni kwamba sasa hivi hakuna uhalifu Dar es Salaam, Tanga, Mwanza pamoja na Kibiti ni shwari, watu waende Kibiti wakalime, wakaweke viwanda sasa hivi kibiti 'guest house' zimepanda", amesisitiza.
Katika hatua nyingine ACP Mwakalukwa ametaja sababu kubwa ya watu kujichukulia sheria mkononi moja wapo ni wivu wa mapenzi baina ya wanandoa pindi wanapo wagundua 'wagoni' wao huwa wanampigia kelele za wizi na mwishowe kuuwawa.
"Watu tuwaelimishe wawe na moyo wa upendo, zitumike taasisi za kidini kwamba hiyo tabia ni mbaya. Ni kweli anapokuitia mwizi wakati wewe ni mgoni wake utauwawa lakini sababu itakuja kusemwa watu wamejichukulia sheria mkononi na kuificha sababu ya wivu wa mapenzi na kuja kuonekana kitu kingine. kwa hiyo niseme ama niwaagize wananchi kuwa tujue madhara ya kujichukulia sheria mkononi ", amesema ACP Mwakalukwa.

Pamoja na hayo,  ACP Mwakalukwa ameendelea kufafanua kuwa "mauaji ya kujichukulia sheria mkononi watu wengi walikuwa na wazo moja tu kwamba wanauwawa wote ni wale vibaka hapana siyo kweli wapo watu wanaodaina akiona halipwi anaumua kumchoma kisu. Leo hii hatushuhudia vibaka wakichomwa moto lakini tunashuhudia familia zikiuwana", amesisitiza.

Kwa upande mwingine, ACP Mwakalukwa amesema Jeshi la Polisi linapenda ushirikiano baina ya wananchi, waandishi na wadau mbalimbali ili waweze kuzuia kupanda na uharifu.

No comments:

Post a Comment