Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Shirika Hodhi la Reli (RAHCO) Bw. Masanja Kadogosa akielezea jambo mbele
ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
(kushoto) wakati wa ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya Kati
kwa kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) ambapo awamu ya yenye urefu
wa Km 205 inajengwa kutoka Dar – Moro.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akikagua ujenzi wa tuta kwa ajili ya
njia ya reli alipotembelea eneo la Soga (Kibaha) wakati wa ziara yake ya
kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya kiwango cha kimataifa (Standard
Gauge) yenye urefu wa kilomita 205 kutoka Dar – Morogoro leo. Kutoka
kulia ni Meneja Mradi wa SGR Mhandisi Maizo Mgedzi, Meneja wa Kanda ya
Afrika Mashariki wa Kampuni ya Yapi Merkezi Bw. Abdullah Kilic na
Mhandisi Felix Nnalio.
Meneja wa Kanda ya Afrika
Mashariki wa Kampuni ya Yapi Merkezi Bw. Abdullah Kilic akifafanua jambo
kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa
kuhusu ujenzi wa tuta la reli ya kisasa ya SGR alipotembele eneo la
Soga (kibaha) leo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo mbele ya Meneja wa
Kanda ya Afrika Mashariki wa Kampuni ya Yapi Merkezi Bw. Abdullah Kilic
(katikati) alipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Reli ya
kiwango cha kimataifa (Standard Gauge) ambapo awamu ya kwanza inajengwa
kutoka Dar – Moro yenye urefu wa 205km.
Muuonekano wa awali wa tuta la
reli linaloendelea kujengwa kwa kuondolewa tabaka la udongo wa kilimo na
kuwekewa udongo wa ujenzi katika eneo la Soga (Kibaha) ambapo mradi wa
ujenzi wa reli ya kisasa unaendeleo.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akitazama kifaa cha kupima mgandamizo
wa ardhi mara baada ya ardhi kushindiliwa alipokagua ujenzi wa tuta la
reli katika eneo la Soga (Kibaha).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiendelea na shughuli ya ujenzi wa
karakana ya kutengeneza mataluma ya reli alipokagua ujenzi alipofanya
ziara katika eneo la Soga (Kibaha).
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amemtaka Mkandarasi Yapi Merkezi na
Motaengil Africa anayejenga Reli ya kati ya kisasa (Standard Gauge)
sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro kilomita 205 kuhakikisha ujenzi
huo unakamilika ndani ya miezi thelathini iliyopangwa.
Akizungumza mara baada ya kukagua
tuta litakapojengwa reli hiyo kutoka pugu, soga hadi ngerengere profesa
mbarawa amepongeza kazi inayoendelea na kumtaka mkandarasi kuongeza kasi
ili kazi ya kutandika reli ianze katika muda mfupi ujao.
“Hakikisheni kazi ya ujenzi wa
tuta na kiwanda cha kutengeneza mataruma ya zege vinakamilika katika
muda wa miezi mitatu kutoka sasa ili kwenda na ratiba ya ujenzi huo,”
amesema Profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amekagua kiwanda
cha kutengeneza mataruma ya zege yatakayotumika katika ujenzi wa reli
hiyo na kusisitiza umuhimu wa mkandarasi kutoa fursa za ajira kwa
wananchi wanaozunguka reli hiyo.
“Wale mtakaopata ajira katika reli
hii hakikisheni mnafanyakazi kwa bidii na uaminifu ili kuwezesha ukenzi
kuwa katika ubora unaotakiwa na kukamilika kwa wakati”, amesisitiza
profesa Mbarawa.
Profesa Mbarawa amemuagiza
Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Reli (TRL) na Kaimu Mkurugenzi
Mtendaji Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli RAHCO) Bwana Masanja
Kadogosa kuanza mchakato wa kuagiza vichwa vipya vya treni vinavyowiana
na Reli hiyo ili reli itakapokamilika kusiwe na hoja ya kusubiri vichwa
hivyo.
Aidha amesisitiza umuhimu wa TRL
na RAHCO kuandaa wataalam watakaotumika kuendesha Reli hiyo ya kisasa
kwa kuwapatia mafunzo ya kiufundi na kibiashara ili kuhakikisha utendaji
wa Reli hiyo unakuwa wenye tija.
Ujenzi wa Reli ya kisasa ya kati
(Standard Gauge) awamu ya kwanza inayoanzia Dar es Salaam hadi Morogoro
yenye urefu wa Kilomita 205 unatarajiwa kukamilika 2019 na Serikali
inaendelea na juhudi za kuhakikisha inapata fedha ya Ujenzi wa sehemu ya
Morogoro-Dodoma.
Zaidi ya Kilomita 2600 za Reli ya
Kisasa (Standard Gauge) ZINATARAJIWA kujengwa kutoka Dar es Salaam
–Morogoro-Dodoma –Tabora-Isaka-Mwanza na Tabora –Kaliua-Kigoma ili
kuiunganisha Tanzania nan chi jirani na hivyo kuboresha huduma za
uchukuzi na biashara.
Imetolewa na kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
No comments:
Post a Comment