Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe William Lukuvi
amesema mtu yoyote asiyelipa kodi ya ardhi na kuendeleza ardhi hiyo, ni
sababu tosha ya kunyang'anywa ardhi hiyo pamoja na kufutiwa hati ya
umiliki kwa kuwa anaingizia hasara serikali
Waziri Lukuvi amebainisha hayo ikiwa imepita siku moja tokea kwa
aliyekuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tatu, Mh. Fredrick Sumaye kudai chanzo
cha kupokonywa shamba lake ni siasa tu za yeye kuhama chama cha CCM na
kwenda kuupa nguvu upinzani.
Akiongea kuhusu mashamba na viwanja kuchukuliwa Waziri Lukuvi amesema,
"Kila mtu atambue iwe ni kiwanja au shamba kama unatabia ya kutolipa
kodi ya ardhi ni sababu tosha ya wewe kunyang'anywa shamba lako au ardhi
unayomiliki".
Akiendelea kuongea Waziri Lukuvi amesema
"Imejitokeza kwa watu wachache kuchukua ardhi kubwa kwa miaka mingi
kuliko hata uwiano wa uendelezaji wa ardhi hiyo, kwa mfano kuna hati
moja hapa ambayo inapigiwa kelele tokea mwaka 1939 imekuwa ikitembea
mikono mwa watu. Sasa miaka ile watu walikuwa wachache unapokwenda
kuchukua ardhi ya kijiji hekari elfu 60 kwa mfano hivi sasa wananchi
utakuwa umewaachia kitu gani?"
Pia Waziri Lukuvi amesema imekuwa kawaida ya baadhi ya watu wanapowahi
maeneo huwa wanakimbilia kuchukua sehemu zenye manufaa makubwa kwa
upande wao na mwishowe wanashindwa kuendelezaa maeneo hayo kama
walivyoyakimbilia.
"Unawahi kuchukua sehemu zenye manufaa kama mto, ardhi inayolimika, sasa
unachukua hekari zote hizo halafu huliendelezi mwishowe shamba hilo
hilo tunalikuta Benki umelikopea fedha. Kisha umepata fedha hizo
unakwenda kujengea 'apartment' sehemu nyingine na kule wananchi
wanalimezea mate.Serikali wanatumia nguvu kubwa sana kutuliza wananchi
wasivamie hilo shamba , halilimwi, serikali hatupati kodi", alisisitiza
Lukuvi.
Kwa upande mwingine, Waziri Lukuvi amesema serikali imekuwa na huruma
kwa miaka mingi kwa wananchi wake lakini serikali ya uongozi huu
wamekubaliana kila mtu afuate sheria anazo paswa kuzifuata.
No comments:
Post a Comment