Mshambuliaji
wa Klabu ya Fc Monaco, Kylian Mbappe anatarajiwa kukamilisha usajili
wake wa mkopo na klabu ya Ufaransa Paris Saint-Germain (PSG).
Mchezaji huyo anatarajiwa kutua nchini Ufaransa siku ya Leo, kwa mujibu wa ripoti za vyombo vya habari vya Ufaransa.
Kituo cha redio cha Ufaransa siku
ya Jumapili kiliripoti kuwa PSG wamekubali kulipa euro milioni 180
ambazo sawa na dola za marekani 215,000,000) ikiwa ni pamoja na mafao
kwa mshambuliaji huyo mwenye miaka 18.
Usajili huo utaweka historia
katika uhamisho kuwa usajili wa pili wa gharama kubwa zaidi katika soka
baada ya Neymar, ambaye alijiunga na PSG kutoka Barcelona kwa euro
milioni 222 mapema mwezi huu.
Hata hivyo kuna wasiwasi zaidi
kuhusiana na kile kilicho juu ya mkutano wa UEFA wa Fedha unaohusu
gharama kubwa katika usajili wa wachezaji Fair Play (FFP) na ndio maana
PSG wanataka kwanza kumsajili kwa mkopo Mbappe .
Monaco na PSG siku ya Jumapili zilifikia makubaliano ya Kylian Mbappe kwenda PSG kwa gharama ya usajili wa euro milioni 180.
No comments:
Post a Comment