Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja
Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakitiliana sini mkataba wa kitabibu
kwa ajili ya huduma za matibabu ya VVU/UKIMWI nchini Tanzania.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja
Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakibadilishana nyaraka mara baada
ya kusaini kwa ajili ya huduma za matibabu ya VVU/UKIMWI nchini
Tanzania.
Kaimu Balozi wa Marekani nchini
Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja
Generali (Dk.) Denis Raphael Janga wakipiga picha ya pamoja na maofisa
wa Ubalozi wa Marekani na Jeshi la Wananchi JWTZ mara baada ya kusiniana
mkataba huo.
Serikali ya Marekani kupitia Taasisi ya kijeshi ya Walter Reed
(WRAIR) imesaini upya makubaliano ya ushirikiano na Jeshi la Wananchi
wa Tanzania (JWTZ) siku ya Jumanne, Agosti 29, 2017 katika sherehe ya
kusaini tamko la pamoja la ushirikiano katika jitihada za kupambana na
VVU/UKIMWI. WRAIR ni kitengo cha kikosi cha jeshi la Marekani
kinachojihusisha na tafiti za kitabibu na kimefanya kazi moja kwa moja
na JWTZ tangu mwaka 2004 kutekeleza programu za VVU/UKIMWI Tanzania.
Utiaji saini huo uliofanywa na
Kaimu Balozi wa Marekani nchini Tanzania Dr. Inmi Patterson na Mkuu wa
Huduma za Kitabibu wa JWTZ, Meja Generali (Dk.) Denis Raphael Janga,
unawakilisha dhamira ya pamoja katika upatikanaji endelevu wa huduma za
afya na mpango mkakati wa kukabiliana na tishio la VVU/UKIMWI.
Makubalino ya awali,
yaliyosainiwa mwaka Aprili 2011 yanabainisha ushirikiano wa pande hizo
mbili katika kupunguza maambukizi mapya na kuboresha matibabu na huduma
za kuzuia maambukizi.
Kupitia ushirikiano huu endelevu
wa pande hizi mbili Mfuko wa Dharura wa Rais wa Marekani wa Kupambana na
UKIMWI (PEPFAR) unatoa nafasi kwa majeshi ikiwemo JWTZ kuelewa vizuri
tishio la afya, tabia na mazingira hatarishi yanayohusiana na kuenea kwa
maambukizi ya VVU.
“Mafanikio ya ushirikiano wa
WRAIR/JWTZ hayapingiki na faida zake ziko wazi.”alisema Kaimu Balozi
Patterson. “Kwa pamoja tumehakikisha upatikanaji endelevu wa huduma za
tiba kupitia ujenzi wa vituo vipya, ukarabati wa vituo vya zamani, vya
matunzo na tiba na kutoa vifaa vya maabara.”
Ushirikiano huu wa pande mbili
kati ya WRAIR na JWTZ umeundwa kuimarisha na kusaidia utafiti na
utekelezaji wa jitihada za matunzo na matibabu ya VVU nchini Tanzania.
No comments:
Post a Comment