Thursday, 24 August 2017

Taarifa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza

Image result for ahmed msangi
TAARIFA YA JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA KWA VYOMBO
VYA HABARI LEO TAREHE 24.08.2017
  • WATU WATATU WAMEFARIKI DUNIA KATIKA AJALI ILIYOHUSISHA KUGONGANA KWA `MAGARI MATATU WILAYANI KWIMBA.
KWAMBA TAREHE 22.08.2017 MAJIRA YA SAA 19:30 HRS USIKU  KATIKA BARABARA  YA MWANZA KWENDA SHINYANGA KWENYE KIJIJI CHA HUNGUMALWA WILAYA YA KWIMBA MKOA  WA MWANZA, GARI NAMBA T.532  CXE AINA YA ZHONGTON BUS  MALI YA FRESTER LIKITOKEA MWANZA KUELEKEA KAHAMA LIKIENDESHWA NA DEREVA ALIYEFAHAMIKA KWA JINA LA JAFURU OMARY, MIAKA 32, MKAZI WA NZEGA – TABORA, LIKIWA KWENYE MWENDO KASI LILIGONGA TREKTA LENYE NAMBA T.433 DFD AINA YA FIATI, MALI YA PETER NDEGE MKAZI WA HUNGUMALWA NA KISHA BUS HILO LILIHAMA NJIA NA KUGONGANA USO KWA USO NA GARI LENYE NAMBA T.349 CAX AINA YA SCANIA LORI MALI YA MWANZA HUDUMA NA KUSABABISHA VIFO KWA WATU WATATU AMBAO NI 1. DEREVA WA BUS HILO JAFURU OMARY, MIAKA 32, 2.BOLE ELKANA, DEREVA WA SCANIA LORI, ANAYEKADIRIWA KUWA NA UMRI KATI YA MIAKA 45 HADI 5, MKAZI WA MWANZA NA 3. ABIRI WA BUS AMBAYE HADI SASA JINA LAKE BADO HALIJAFAHAMIKA NA KUSABABISHA MAJERUHI KWA ABIRIA KUMI NA MBILI (12).
INADAIWA KUWA DEREVA WA BUS HILO AINA ZHONGTON ALIKUWA KWENYE MWENDO KASI NA ALIPOFIKA MAENEO TAJWA HAPO JUU ALIKUTANA NA TREKTA NDIPO ALISHINDWA KUSHIKA BREKI NA KUPELEKEA KUGONGA TREKTA KWA NYUMA HALI ILIYOPELEKEA BUS HILO KUHAMA NJIA NA KUGONGANA USO KWA USO NA GARI LINGINE AINA YA SCANIA LORI NA KUPELEKEA VIFO KWA MAREHEMU TAJWA HAPO JUU NA MAJERUHI KUMI NA MBILI.

CHANZO CHA AJALI NI MWENDO KASI WA DEREVA WA BUS AINA ZHONGTON HALI ILIYOPELEKA DEREVA HUYO KUSHINDWA KULIMUDU BUS NA KUPELEKEA KUSHINDWA KUSHIKA BREKI NA KUSABABISHA AJALI ILIYOSABABISHA VIFO NA MAJERUHI. MAJERUHI SABA (07) WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA NA MAJERUHI WENGINE WATANO (05) WAMELAZWA HOSPITALI YA WILAYA YA MISUNGWI WAKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU NA HALI ZAO ZINAENDELEA VIZURI. MIILI YA MAREHEMU IMEHIFADHIWA HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA KWA AJILI YA UCHUNGUZI NA UTAMBUZI, PINDI UCHUNGUZI UKIKAMILIKA ITAKABIDHIWA KWA NDUGU WA MAREHEMU KWA AJILI YA MAZISHI.
KAMANDA WA POLISI MKOA WA MWANZA NAIBU KAMISHINA WA POLISI AHMED MSANGI ANATOA WITO KWA MADEREVA KUWA WASIHITAJI KUSHURUTISHWA PINDI WAWAPO BARABARANI BALI WANATAKIWA WATAMBUE KUWA WANAWAJIBU WA KUTII SHERIA, KANUNI NA TARATIBU ZA USALAMA BARABARANI ILI KUEPUSHA VIFO NA MAJERAHA KWA WATU WASIO NA HATIA.
IMETOLEWA NA:
DCP: AHMED MSANGI.
KAMANDA WA POLISI (M) MWANZA

No comments:

Post a Comment